Gor Mahia yalalamikia kupangwa na Pyramids

Droo ya CAF Champions League 2026/27 imezua mjadala mkubwa nchini Kenya baada ya Gor Mahia kupewa Pyramids FC ya Misri kama mpinzani wao katika raundi ya kwanza ya hatua ya awali.Mashabiki na baadhi ya wanahabari wa michezo nchini humo wameeleza kutoridhishwa na droo hiyo, wakidai kuwa kipimo walichopewa Gor Mahia ni kikubwa mno kwa hatua ya kwanza ya mashindano.

Kwa mtazamo wao, kuipanga Gor Mahia na mabingwa wa Afrika wa mwaka 2025 katika raundi ya kwanza ni changamoto kubwa sana, hasa kwa klabu inayolenga kusonga mbele hadi hatua ya makundi.Baadhi ya sauti kutoka Kenya zimeenda mbali zaidi kwa kuuliza iwapo CAF kweli inataka Gor Mahia isonge mbele katika mashindano hayo.

Hoja yao kubwa ni kwamba:"Kama CAF haikuwa na nia ya kutaka Gor Mahia ifuzu hatua inayofuata, ingesema mapema tu!"Hata hivyo, licha ya malalamiko hayo, droo tayari imepangwa na Gor Mahia sasa inakabiliwa na kazi kubwa dhidi ya Pyramids FC. Ni vita ya Gor Mahia dhidi ya bingwa wa Afrika na K’Ogalo sasa inahitaji kuonyesha uwezo wake ndani ya uwanja.


Machapisho maarufu kutoka blogu hii

FIFA yatoa orodha ya vilabu bora duniani, Simba na Yanga zachuana vikali

Kocha Simba anataka wachezaji wapya watano

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI