Girumugisha awasifu viongozi wa Yanga
Baada ya Jean Claude Girumugisha kujiunga na klabu ya Al Ahli Tripoli ya nchini Libya ameweka wazi jinsi ambavyo dili lake la kujiunga na klabu ya Yanga liliikwama, huku akiwamwagia sifa mabosi wa Yanga.
"Ni kweli Yanga walinitaka na nilikuwa tayari kwenda.Nilifurahishwa sana na namna viongozi wao walivyoniheshimu na walivyokutana na mimi,Tatizo lilikuja kwenye maslahi ya klabu kwa klabu. Kulikuwa na mambo ambayo yalihitaji makubaliano kati ya Al Hilal na Yanga, hivyo haikuwezekana kumaliza kila kitu,"
"Pengine baadaye nitakuja Tanzania, nilipenda mabosi wa Yanga walivyozungumza na mimi kwa heshima kubwa."
-Jean Claude Girimugisha (Akielezea jinsi ambavyo dili lake kujiunga na Yanga lilivyokwama na kutua Al Ahli Tripoli)
