Edo Kumwembe amfananisha kocha wa Yanga na Mourinho
Mchambuzi wa soka nchini, Edo Kumwembe, kupitia ukurasa wake wa Instagram amemnukuu na kumpa ujumbe mzito mchezaji 'Chuga Boy' pamoja na mtindo wa ukocha wa Yanga SC:
"Huyu wa Yanga kama sio tabia zake binafsi basi atakuwa amewachagua akina Mourinho wawe mfano wake. Wanakuchana hapo hapo. Uwe mchezaji wake au Mwandishi wa habari."
"Alichofanywa Chuga boy ndio ajifunze kucheza chini ya makocha tofauti. Lakini jambo la msingi katika hili ni kwamba aliambiwa ukweli. Alijaribu kucheza na Jukwaa wakati kule mbele Yanga wanacheza mpira rahisi ndio maana wanatengeneza nafasi nyingi."
"Kijana ana kipaji kikubwa asiwe na haraka ya kuthibitisha. Siku hizi tunahesabu zaidi pasi, Assists na mabao. Chenga nyingi tuliacha."
