Depu mbioni kwenda Petro de Luanda

Taarifa za ndani zinaeleza kuwa klabu ya Petro de Luanda ya Angola imepiga hatua kubwa katika harakati za kumsajili mshambuliaji wa Young Africans, Aurélio Depu (26).

Inaelezwa kuwa klabu hiyo imeweka mezani kiasi cha takribani KZ milioni 455 (sawa na karibu Shilingi bilioni 1.3 za Kitanzania) ili kufanikisha usajili wa nyota huyo.

Mbali na ada ya usajili, Petro de Luanda inadaiwa kumpatia Depu mkataba wa miaka miwili wenye kipengele cha kuongeza mwaka mmoja zaidi endapo pande zote zitaridhishwa na utendaji wake.

Vyanzo vinaongeza kuwa hakuna tofauti kuhusu maslahi binafsi kati ya mchezaji huyo na Petro de Luanda, huku Young Africans ikionekana kuwa tayari kusikiliza ofa kwa ajili ya kumruhusu kuondoka.

Iwapo dili hilo litakamilika, Aurélio Depu anatarajiwa kuwa mchezaji anayelipwa mshahara mkubwa zaidi ndani ya kikosi cha Petro de Luanda.

Depu anampisha beki kisiki aliye tambulishwa leo Bukombe GEITA Komara kutoka Ivory coast.


Machapisho maarufu kutoka blogu hii

FIFA yatoa orodha ya vilabu bora duniani, Simba na Yanga zachuana vikali

Kocha Simba anataka wachezaji wapya watano

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI