Clatous Chama atangaza kustaafu
Mwamba wa Lusaka, Clatous Chota Chama, ametangaza rasmi kustaafu kuchezea Timu ya Taifa ya Zambia Chipolopolo, akihitimisha safari yake ndefu na ya mafanikio katika soka la kimataifa.
Chama, ambaye kwa sasa yupo nchini Rwanda na kikosi cha Simba SC kwa ajili ya kambi ya maandalizi ya msimu mpya, amebainisha kuwa umefika wakati sahihi wa kutundika daluga katika ngazi ya taifa na kuweka umakini wake wote kwenye soka la klabu.
