Bodi ya Ligi yapiga mkwara matumizi ya FVS
Kamati ya Bodi ya Ligi imezikumbusha timu zote kuzingatia kikamilifu Kanuni ya 20 inayohusu matumizi ya Teknolojia ya Football Video Support System (FVS).
Kwa mujibu wa Kanuni ya 20(4), Kocha Mkuu au kiongozi mwingine wa juu kwenye benchi la ufundi ndiye mwenye mamlaka ya kuwasilisha ombi la marejeo ya tukio kupitia Mwamuzi wa Akiba.
Mchezaji akiona tukio linahitaji marejeo ya FVS, anatakiwa kumjulisha Kocha Mkuu au kiongozi wa benchi kwa ishara, ili kiongozi huyo awasilishe ombi hilo.Bodi ya Ligi imeonya kuwa mchezaji haruhusiwi kumlalamikia au kumshinikiza mwamuzi moja kwa moja ili kuomba marejeo ya FVS.Mchezaji atakayekiuka utaratibu huo ataadhibiwa kwa mujibu wa Kanuni ya 17:62.
