Yanga Princess ni nyumbani nimeamua kurudi- Precious

KIUNGO wa kimataifa kutoka Nigeria, Precious Christopher, amesema kurejea kwake Yanga Princess ni kama kurudi nyumbani baada ya kutambulishwa rasmi na klabu hiyo jana jijini Dar es Salaam.
-
Kupitia ukurasa wake wa mitandao ya kijamii, Precious aliandika: “Nyumbani!! Nyumbani!! Nyumbani!! Aya ndugu zangu nimesikiliza na nimerudi nyumban, Mimi siku zote ni Mwananchi,"
-
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 22 aliwahi kuichezea Yanga Princess kabla ya kusajiliwa na Simba Queens msimu uliopita, ambako alisaini mkataba wa miaka miwili na kuonesha kiwango bora akiwa kiungo mkabaji mwenye nguvu na pasi sahihi.
-
 Msimu uliopita alifunga mabao matatu na kutoa pasi ya bao moja katika Ligi Kuu ya Wanawake Tanzania (WPL).
-
Mbali na Precious, Yanga Princess pia wamemtambulisha kiungo mwingine mpya, Ritticia Nabossa kutoka Uganda, ambaye awali alicheza Fountain Gate Princess kisha kujiunga na Simba Queens na Wincate Kaari.
-
Nabossa ni miongoni mwa wachezaji tegemeo wa timu ya taifa ya wanawake ya Uganda (Crested Cranes) na amewahi kushinda Ngao ya Jamii ya Wanawake  akiwa na Simba.

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

FIFA yatoa orodha ya vilabu bora duniani, Simba na Yanga zachuana vikali

Beno Ngassa mdogo wa Mrisho Ngassa anayekipiga Tanzania Prisons

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI