Aliyekuwa Mkurugenzi wa Ufundi na Kocha Msaidizi wa Klabu ya Yanga Sc Abdulhamid Moalin hatokuwa sehemu ya kikosi cha Mabingwa hao wa Ligi Kuu bara msimu wa 2024/26 baada ya mkataba na waajiri wake hao kufikia ukomo.
Moalin ambaye alijiunga na Yanga akitokea KMC katikati ya msim uliopita ameujulisha uongozi wa Yanga juu ya dhamira yake ya kutoongeza mkataba huku klabu hiyo ikibariki matakwa hayo baada ya kocha mpya Romain Folz kuhitaji kuwa na benchi lake binafsi.
Taarifa zaidi zinaeleza kuwa Moalin na aliyekuwa mchambuzi wa video (video analyst) wanatarajiwa kujiunga na aliyekuwa kocha wa Yanga Sc Sead Ramovic kunako klabu ya CR Belouzidad.