Lassine Kouma atambulishwa Yanga

KLABU ya Yanga imemtambulisha kiungo chipukizi wa Kimataifa wa Mali, Lassine Kouma (21) kuwa mchezaji wake mpya kuelekea msimu ujao 2025-2026.

Kouma anasaini mkataba wa kujiunga na mabingwa wa Tanzania akitokea Stade Malien ya kwao, Bamako.

Kouma ni mchezaji anayeweza kucheza kama kiungo wa ulinzi, winga, kiungo wa katikati, kiungo mshambuliaji na mshambuliaji wa katikati.

Anakuwa mchezaji mpya wa nne Yanga SC na wa pili tu wa kigeni baada ya kiungo mwingine wa Kimataifa wa Guinea, Balla Mousa Conte kutoka CS Sfaxien ya Tunisia.

Wengine ni wazawa wawili kiungo Abdulnasir Mohamed Abdallah kutoka Mlandege ya Zanzibar na winga Offen Francis Chikola kutoka Tabora United.

Aisha, Yanga pia imeajiri kocha mpya Mkuu, Mfaransa Romain Folz mwenye asili ya Morocco ambaye amekuja na Msaidizi mmoja, Kocha wa Makipa. Majdi Mnasria.


Machapisho maarufu kutoka blogu hii

FIFA yatoa orodha ya vilabu bora duniani, Simba na Yanga zachuana vikali

Beno Ngassa mdogo wa Mrisho Ngassa anayekipiga Tanzania Prisons

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI