Inaripotiwa kuwa Yanga SC wamepokea USD 350,000 (Tsh milioni 945) kutoka Wydad Casablanca kama sehemu ya kumnunua Azizi Ki aliyekuwa amesalia Mkataba wa mwaka mmoja Jangwani.
Aziz Ki amepewa USD 150,000 (Tsh million 405) kama ada ya usajili kutokea Wydad na kusaini Mkataba wa miaka miwili.
Wydad wamempa ofa ya mshahara mara mbili ya aliyokuwa anapewa Yanga na sasa analipwa USD 40,000 (Tsh milioni 107) kutoka USD 20,000 (Tsh milioni 53) aliyokuwa analipwa na Yanga SC.
Kama ndivyo basi Stephano amezidi kukuwa toka ametoka Asec amekuwa akikua kiuchumi kila anaposaini Mkataba mpya.