Wydad Casablanca yamtambulisha Aziz Ki

KLABU ya Wydad Athletic imemtambulisha rasmi kiungo mshambuliaji wa Kimataifa wa Burkina Faso, Stephane Aziz Ki kuwa mchezaji mpya baada ya kukamilisha uhamisho wake kutoka Yanga ya Tanzania.

Utambulisho huo umefanyika usiku wa kuamkia leo – saa chache tu baada ya Yanga kumuaga Aziz Ki kufuatia kuwa naye kwa misimu mitatu tangu awasili kutoka ASEC Mimosas.

Wydad Athletic ya Morocco na usajili wake umeharakishwa ili akacheze michuano ya Klabu Bingwa ya Dunia ya FIFA inayotarajiwa kuanza Juni 14 hadi Julai 13 nchini Marekani ikishirikisha timu 32 kutoka Mabara sita – nne kutoka Afrika, nyingine ni Al Ahly ya Misri, EspĂ©rance ya Tunisia na Mamelodi Sundown ya Afrika Kusini.


Machapisho maarufu kutoka blogu hii

FIFA yatoa orodha ya vilabu bora duniani, Simba na Yanga zachuana vikali

Beno Ngassa mdogo wa Mrisho Ngassa anayekipiga Tanzania Prisons

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI