Kufuatia kauli aliyoitoa mwenyekiti wa Bodi ya Ligi Ndugu Steven Mguto kuhusu sakata la dabi, alisema kuwa tarehe ya Dabi ipo pale pale na kusisitiza kuwa hiyo kauli ya "HATUCHEZI" wao kama Bodi haiwezi kubadili maamuzi waliyoyapanga.
Kamati ya WAZEE wa Yanga kupitia kwa Mwenyekiti wa Baraza hilo Mohammed Msumi amesema "Sisi Yanga hatuna shida na mtu yoyote lakini tunasisitiza kuwa HATUTASHIRIKI MCHEZO WA DABI hiyo Tarehe 15 mpaka haki ipatikane"
"Kwanza watujibu hoja zetu 3 ,ili suluhu ipatikane, Vinginevyo hakuna kiongozi yoyote anaweza kutuamrisha,haijalishi ni kiongozi wa Bodi au wa serikali"
"Kuhusu kikosi chetu hatuna wasiwasi wowote na wala hatuwaogopi Simba kwasababu tumewafunga mara 4 mfululizo"
"Tunachotaka Sheria na kanuni zilizowekwa zisimamiwe ,na kama wao Bodi ya Ligi ndiyo wamekosea basi watoke Hadharani kuuomba umma radhi"
MOHAMMED MSUMI M/kiti Baraza la Wazee Young Africans SC