Simba yaihofia Singida Black Stars kesho

“Mechi ya Singida ni mechi ya kiporo na haiwezi kuwa rahisi, Singida ni moja ya timu ngumu sana, timu ambayo imewekeza, ina wachezaji wazuri, timu ambayo katika ligi inasumbua ila sisi kama Simba tumejipanga, pamoja na ugumu wao Singida lazima tupate matokeo ya alama tatu kesho”

''Suala la rotation lipo chini yetu waalimu, kwahiyo tutaangalia baada ya mazoezi ya leo, kikubwa ni kwamba timu nzima ipo kambini na wachezaji wote wapo vizuri, ni suala la benchi la ufundi kuona nani aanze na nani asianze.

Fainali imeisha licha ya suala la saikolojia baada ya kupoteza mchezo wa fainali halikuwa sawa ila wachezaji wetu ni wakomavu baada ya fainali tulisema kwamba hili limekwisha, targate yetu sasa ni kuhakikisha tunapta kikombe Ligi kuu na hatuwezi kuwa mabingwa kama hatutoshinda mchezo wa kesho” - Seleman Matola Kocha Msaidizi Simba SC