Simba kuadhibiwa na CAF


Kwa taarifa za awali ni kuwa Shirikisho la soka barani Afrika (CAF) lipo kufanya uchunguzi juu ya matukio mbalimbali kabla ya fainali mkondo wa kwanza na baada ya fainali ya mkondo wa pili ambapo kuna uwezekano mkubwa Simba ikakumbwa na rungu la Shirikisho hilo kutokana na mienendo ya Mashabiki wake lakini pia baadhi ya Viongozi Waandamizi wakumbana na adhabu kali, inatajwa hivyo kufuatia mtiririko wa matukio mbalimbali katika fainali hiyo.
.
Taarifa za awali zinadai pia kuna matamko na press mbalimbali za kulishutumu CAF kuhusiana na mabadiliko ya uwanja, hivyo wameanza rasmi kukusanya taarifa hizo ili kufanya maamuzi yake ikitajwa ni kuishutumu CAF na kutoa kauli za kichochezi dhidi ya Shirikisho hilo.
.