Rasmi, kocha wa Orlando atambulishwa Al Ahly

KOCHA Mspaniola, José Luis Riveiro jana alitambulishwa kuwa Kocha mpya wa Al Ahly ya Misri wiki mbili tu baada ya kuondoka Orlando Pirates ya Afrika Kusini.

Mara moja Riveiro anapewa jukumu la kwenda kuiongoza Al Ahly katika michuano ya Klabu Bingwa ya Dunia ya FIFA inayotarajiwa kufanyika nchini Marekani hivi karibuni.

Ahly, kati ya wawakilishi wenne wa Afrika pamoja na Wydad Athletics ya Morocco, Esparence ya Tunisia na Mamelodi Sundowns ya Afrika Kusini – ipo Kundi A pamoja na wenyeji, Inter Miami, Palmeiras ya Brazil na FC Porto ya Ureno.


Machapisho maarufu kutoka blogu hii

FIFA yatoa orodha ya vilabu bora duniani, Simba na Yanga zachuana vikali

Beno Ngassa mdogo wa Mrisho Ngassa anayekipiga Tanzania Prisons

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI