Mukwala akamatiki

WENYEJI, Simba SC wameibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Singida Black Stars katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara jioni ya leo Uwanja wa Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni, KMC Complex, Mwenge, Dar es Salaam.

Pongezi kwa mfungaji wa bao hilo pekee, mshambuliaji wa Kimataifa wa Uganda, Steven Dese Mukwala dakika ya 43 akimalizia kazi nzuri ya kiungo Muivory Coast, Jean Charles Ahoua na kwa ushindi huo, Simba SC inafikisha pointi 72, ingawa inabaki nafasi ya pili ikizidiwa pointi moja tu na mabingwa, Yanga baada ya wote kucheza mechi 28.


Machapisho maarufu kutoka blogu hii

FIFA yatoa orodha ya vilabu bora duniani, Simba na Yanga zachuana vikali

Beno Ngassa mdogo wa Mrisho Ngassa anayekipiga Tanzania Prisons

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI