Injinia Hersi awajibu Simba

Rais wa klabu ya Yanga, Injinia Hersi Said amewajibu wale walikuwa wakimshambulia mtandaoni kwamba kukaa kwake kimya si kuwaogopa isipokuwa anawavutiwa pumzi na sasa amewapa makavu.

Wacha nieke hiki kitu wazi, kua kiongoz haimaanishi ukubali kejeli na matusi ya kila aina ya watu, kuna sehem unapaswa ukae kimya ila kuna mda uwape kile wanachokitaka.

Wasichokijua wengi ni kwamba mm pia nmetokea maisha ya mtaani, nmeishi na wahuni, nmeishi uswahilini kwahyo ukija vibaya na unikute niko vibaya jibu utalipata.

Kwa sababu wabongo mnahisi matusi ni dawa...ukija kweny page yngu na matusi usitegemee busara kwa sababu na mm ni binadam..mnalaumu sana sijafika uwanjani , hiv kitendo cha kuwafukuza mashabiki wa Yanga eti shughuli sio yao, sasa mimi shughuli ni yangu, hamjitambui..
#daimambelenyumamwiko, aliandika katika ukurasa wake