Hersi aipongeza RS Berkane kwa kushinda ubingwa Afrika


Mwenyekiti wa Umoja wa Vilabu Afrika, Eng. Hersi Said anawapongeza sana Klabu ya RS Berkane kwa kubeba Ubingwa wa Kombe la Shirikisho la Afrika, siku ya jana Mei 25,2025, katika Uwanja wa New Amaan Complex, Zanzibar.

Berkane walibeba Ubingwa huo baada ya kuichapa Klabu ya Simba kwa jumla ya Mabao 3-1, Huku Klabu ya Simba ikiweka aibu ya ikipiga Shuti moja tu Lililolenga Lango [Shots On Target] ndani ya Dakika 180 za mechi za Fainali.

Aidha, Eng Hersi amesisitiza kuwa, Pongezi zake kwa Timu Afrika atazitoa kwa mabingwa tu na si vinginevyo.


Machapisho maarufu kutoka blogu hii

FIFA yatoa orodha ya vilabu bora duniani, Simba na Yanga zachuana vikali

Beno Ngassa mdogo wa Mrisho Ngassa anayekipiga Tanzania Prisons

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI