Aziz Ki si sehemu ya kikosi Wydad kinachocheza na Sevilla


Kiungo Stephen Aziz Ki sio sehemu ya kikosi cha Wydad Casablanca ambacho kinacheza leo dhidi ya Sevilla ya Hispania.

Mshambuliaji Mtanzania Selemani Mwalimu 'Gomez' yupo kwenye kikosi cha Wydad ambacho kinaivaa Sevilla leo usiku.

Mechi hiyo ni sehemu ya maandalizi ya Wydad kwa ajili ya michuano ya Klabu Bingwa ya Dunia ya FIFA 2025 inayotarajiwa kufanyika nchini Marekani kuanzia Juni 15 hadi Julai 13.

Taarifa zaidi zinasema kwamba pamoja na mechi dhidi ya Sevilla ambao waliwasili jana Casablanca – Wydad pia watacheza na FC Porto ya Ureno Jumapili kukamilisha mbili za kirafiki kabla ya Klabu Bingwa ya Dunia.