Arajiga kuchezesha Simba na Singida Black Stars nusu fainali kesho


Kwa mujibu wa taarifa za ndani kutoka vyanzo vya kuaminika, Mwamuzi wa Kimataifa kutoka Tanzania, Ahmed Arajiga, ameteuliwa rasmi kuchezesha mchezo wa Nusu Fainali ya Kombe la CRDB (CRDB Federation Cup) kati ya miamba wa soka la Tanzania, Simba SC na Singida Black Stars.

Mchezo huo wa kusisimua unatarajiwa kupigwa kesho kwenye Uwanja wa Tanzanite (Kwara), ukiwa ni moja ya mechi ngumu na za kuvutia zaidi kwenye ratiba ya msimu huu wa michuano ya CRDB.

Kuteuliwa kwa Arajiga kuamua mchezo huu ni uthibitisho wa kuaminiwa kwa muamuzi huyo kwenye mechi za presha na zenye mvutano mkubwa. Simba SC wanaingia wakiwa na rekodi ya mafanikio katika michuano hii, huku Singida Black Stars wakisaka nafasi ya kuandika historia kwa mara ya kwanza.

Mchezo huu utatoa mshindi atakayekutana na Yanga SC kwenye Fainali ya Kombe la CRDB, baada ya Yanga kufuzu mapema na kuweka rekodi ya kufika fainali nyingine tena mfululizo.