Klabu ya APR FC ya Jeshi nchini Rwanda imetwaa kombe la Ligi Kuu nchini humo baada ya kupata ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Muhanzi United.
APR FC imetwaa taji hilo wiki ya 29 ya Ligi Kuu ukiwa umesalia mchezo mmoja. Upande wa pili Rayon Sports walikuwa wenyeji wa Vision FC kwenye Uwanja wa Pele mjini Kigali bila Mashabiki ambapo walitoka sare ya 0-0 na kufikisha pointi 60 huku APR FC ikifikisha alama 64.
Kwa ujumla ,APR FC imeshinda mataji 23 ya Ligi Kuu katika historia yake huku pia ikishinda taji la Amani 2025 na kurudisha rekodi ya kushinda Makombe mawili katika msimu mmoja baada ya kufanya hivyo mwaka wa 2014.