TIMU ya Al Ahly imefanikiwa kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu ya Misri kwa mara ya 45 baada ya ushindi wa mabao 6-0dhidi ya Pharco FC Uwanja wa Cairo International Jijini Cairo.
Ilikuwa siku nzuri kwa mshambuliaji wa Kimataifa wa Palestina, Wessam Abou Ali aliyefunga mabao manne katika mchezoo huo dakika za 10, 33, 61 na 66, huku mabao mengine yakifungw ana Hussein El Shahat dakika ya 75 na Emam Ashour dakiika ya 90’+3.
Ushindi huo umeifanya Al Ahly kumaliza msimu ikiwa na pointi 58, mbili zaidi ya Pyramids FC, ambao waliilaza Ceramica Cleopatra mabao 5-1 lakini wakaambulia patupu.
Mashetani Wekundu walianza msimu huu chini ya Marcel Koller, lakini ni kocha wa muda Emad El-Nahhas ambaye aliwaongoza hadi hatua ya mwisho, na kupata ushindi mara sita mfululizo na akitumia mwanya wa kuteleza kwa Pyramids kutwaa taji hilo.