Mabingwa wa zamani wa kombe la Muungano, Yanga SC wamefanikiwa kutinga hatua ya fainali baada ya usiku huu kuifunga Zimamoto Kwa mikwaju ya penalti 3-0 kufuatia sare ya kufungana bao 1-1 uwanja wa Gombani Pemba.
Yanga walitangulia kupata bao kupitia Maxi Nzengeli dakika ya 28 kabla ya Zimamoto kusawazisha dakika ya 70 kupitia Said Mwinyi, mpira ulimalizika baada ya dakika 90 na wakaenda kwenye changamoto ya penalti.
Yanga walipata penalti tatu na Zimamoto walipoteza tatu na mpira ukamalizwa, penalti ya ushindi ilipigwa na Clement Mzize, Yanga sasa watakutana na JKU Alhamisi kilele cha sherehe za Muungano
.