Mabingwa wa Tanzania bara, Yanga SC usiku huu katika uwanja wa Gombani Pemba, imetinga nusu fainali ya kombe la Muungano baada ya kuilaza KVZ mabao 2-0.
Alikuwa Stephanie Aziz Ki kuitanguliza Yanga kwa bao lake la kwanza dakika ya 27 kabla ya Denis Nkane dakika ya 84 kufunga bao la pili ambapo sasa ni kama wameifuata Azam FC nusu fainali.