Timu ya Azam FC ya jijini Dar es Salaam imetolewa katika michuano ya kombe la Muungano baada ya kufungwa mabao 2-1 na JKU ya Zanzibar uwanja wa Gombani Pemba.
Huu ni msimu mbaya kwa Azam FC kwani wameambulia patupu katika mashindano yote waliyoshiriki.
Neva Adelin dakika ya 50 aliifungia JKU bao la kwanza kabla ya Freddy Suleiman kufunga la pili, Yeison Fuentes aliipatia Azam FC bao la kufuatia machozi dakika ya 15 akitangulia kufunga, dakika ya 90 Abdulhalim Masoud wa JKU alioneshwa kadi nyekundu, JKU wameingia fainali na sasa wanasubiri mshindi kati ya Yanga na Zimamoto kesho.
.