Aigle Noir mabingwa Ligi Kuu Burundi

Klabu ya Aigle Noir CS imeibuka Bingwa wa Ligi Kuu Burundi, baada ya kutoka sare ya 0-0 dhidi ya Royal Vision 2026 zikiwa zimebaki mechi mbili ili Ligi iweze kutamatika.

Imetwaa Kombe hilo baada ya Bumamuru FC iliyokuwa ikikimbizana na Aigle Noir CS kupokea kichapo cha mabao 2-0 kutoka kwa Musongati FC ya mkoani Gitega.

Aigle Noir Club Sportif imetangazwa Bingwa ikiwa na pointi 8 mbele ya Bumamuru FC. Baada ya miaka 6, Fighters wanashinda taji lao la pili la Ubingwa wa Ligi Kuu katika historia yao.

Mechi ambazo zimebaki kwa Aigle Noir CS kabla ya Ligi Kuu kumalizika ni dhidi ya Rukinzo FC wiki ya 29 na Inter Stars wiki ya 30.


Machapisho maarufu kutoka blogu hii

FIFA yatoa orodha ya vilabu bora duniani, Simba na Yanga zachuana vikali

Beno Ngassa mdogo wa Mrisho Ngassa anayekipiga Tanzania Prisons

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI