Zidane abwaga manyanga Real Madrid
Baada ya kuiwezesha kutwaa tena taji la Ligi ya Mabingwa barani Ulaya, kocha wa Real Madrid, Zinedine Zidane "Zizzou" ameachia ngazi kuinoa timu hiyo. Taarifa zilizotangazwa na vyombo mbalimbali vya habari barani Ulaya vinasema Zidane ameachia ngazi baada ya kuiwezesha timu hiyo kutwaa taji la tatu Ulaya na moja la La Liga, huku akiwa na rekodi ya kushinda mechi 104 na kutoka sare mara 29 jumla akibeba mataji tisa kwa wakati wote akiwa na Real Madrid. Zidane amesema bado anaipenda Real Madrid na ataendelea kuishabikia katika kipindi chake chote cha maisha ya soka, Zidane amewahi pia kuichezsa klabu hiyo pamoja na timu ya taifa lake ya Ufaransa na kujipatia umaarufu mkubwa enzi zake Zinedine Zidane ameachia ngazi Real Madrid