Wachezaji Singida United wapewa mifuko 50 ya Cement kila mmoja

Na Mrisho Hassan. Arusha

Akizungumza na vyombo vya habari hiii leo,Mkurugenzi wa Singida United Ndg. Festo Sanga amesema, Uongozi wa klabu kuanzia chini ya Rais na mwenyekiti wa timu hiyo wameamua kutoa mifuko ya Cement kwa kila mchezaji na mtumishi wa klabu hiyo kama shukrani na pongezi kwa namna walivyopambana kufanikisha sehemu ya malengo ya klabu kwa msimu wa 2017/2018.

Tukio hilo ambalo kama sila kwanza hapa nchini, basi ni tukio la heshima na upendo wa hali ya juu katika kuimarisha mahusiano ya klabu na wachezaji, Singida United imetoa mifuko hiyo kama alama katika maisha ya wachezaji na watumishi kwamba katika maisha ya soka kuna maisha mengine ya kuanza kujitegemea mapema.

Uongozi wa Singida United umetoa mifuko 50 ya Cement kwa kila mchezaji mmoja na mwalimu wao

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

FIFA yatoa orodha ya vilabu bora duniani, Simba na Yanga zachuana vikali

Beno Ngassa mdogo wa Mrisho Ngassa anayekipiga Tanzania Prisons

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI