Simba yamaliza kwa sare, Majimaji na Njombe zaipa kisogo Ligi Kuu Bara

Na Prince Hoza. Dar es Salaam

Timu ya soka ya Simba Sc ya jijini Dar es Salaam jioni ya leo imemaliza Ligi Kuu Bara kwa heshima ya aina yake baada ya kuilazimisha sare ya kufungana bao 1-1 Majimaji Fc katika uwanja wa Majimaji mjini Songea.

Kwa matokeo hayo Simba imefikisha pointi 69 na ikiwa mabingwa wa Tanzania Bara msimu huu huku timu ya Majimaji ikiwa imetelemka daraja ikiungana na Njombe Mji, Majimaji walikuwa wa kwanza kupata bao kupitia Marcel Kaheza kabla ya Simba kusawazisha kwa penalti kupitia Haruna Niyonzima ambaye pia alikosa penalti iliyotaka kuzaa bao la pili iliyppanguliwa na kipa wa Majimaji, Hashim Mussa.

Matokeo mengine Mbao Fc 1 Ruvu Shooting 1 uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza.

Mtibwa Sugar 0 Mbeya City 0 Uwanja wa Manungu Complex mjini Morogoro.

Kagera Sugar 2 Lipuli 0 uwanja wa Kaitaba mjini Kagera.

Ndanda Fc 3 Stand United 0, Nangwanda Sijaona mjini Mtwara.

Mwadui Fc 2 Njombe Mji 0 Uwanja wa Sabasaba mjini Njombe.

Tanzania Prisons 1 Lipuli 0 Uwanja wa Sokoind mjini Mbeya.

Mpambano mwingine wa kufunga pazia la ligi utafungwa usiku wa leo kati ya Yanga Sc na Azam Fc uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam

Simba imemaliza ligi kwa heshima baada ya kutoka sare na Majimaji 1-1 leo

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA

STAA WETU: JEREMIA JUMA MTOTO WA JUMA MGUNDA ALIYEIKACHA SIMBA NA KUENDELEA NA UASKARI