YANGA YAIFUATA SIMBA ZENJI
Wakati Simba imechagua Zanzibar kuwa kambi yake, kikosi cha cha mabingwa wa Ligi Kuu ya Soka Tanzania Bara, Yanga, nacho kinatarajiwa kwenda kujichimbia mjini humo kwa ajili ya kuweka kambi kujiandaa na msimu mpya wa ligi hiyo itakayoanzia Septemba 12, mwaka huu.
Katibu Mkuu wa Yanga, Jonas Tiboroha, alisema jana kuwa wameamua kwenda visiwani humo ili kujiimarisha kabla ya kuanza kwa msimu mpya wa ligi.
Tiboroha alisema kwamba kambi hiyo itakuwa ya siku saba na lengo ni kuwafanya wachezaji waliobakia nchini kujijenga na kuwa imara tayari kukabiliana na ushindani wa mechi za ligi hiyo.
"Tunataka wachezaji wenzao ambao wako na timu za taifa wakirudi wote wawe fiti kwa ajili ya kushindana ligi itakapoanza," alisema Tiboroha.
Aliongeza kwamba timu ikiwa Zanzibar itafanya mazoezi mara mbili kwa siku na mara baada ya walioko kwenye timu za taifa kurejea ndipo watacheza mechi moja ya kirafiki kabla ya ligi haijaanza.
"Ni ushauri wa benchi la ufundi wanataka wachezaji waliobakia nao wapate mazoezi yanayolingana na wenzao, tumejipanga zaidi na lengo ni kuhakikisha tunakuwa na kikosi imara kuanzia mechi ya kwanza," Tiboroha aliongeza.
Yanga itaanza kutetea ubingwa wake Jumapili ya Septemba 13 mwaka huu kwa kuikaribisha Coastal Union kutoka Tanga mchezo utakaofanyika kwenye Uwanja wa Taifa jijini, Dar es Salaam.