UBINGWA WA AZAM NI HISTORIA NYINGINE CECAFA
Azam imeandika historia mpya kwa kutwaa ubingwa wa Kombe la Kagame bila ya kufungwa bao lolote, baada ya kuichapa Gor Mahia ya Kenya kwa mabao 2-0 jana kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Mabao ya John Bocco na Kipre Tchetche yalitosha kuifanya Azam kutawazwa kuwa ufalme wapya na kufanikiwa kulibakiza kombe hilo katika ardhi ya Tanzania kwa rekodi ya aina yake ya kutoruhusu bao lolote katika michezo yake sita ya mashindano ya Ligi ya Mabingwa Afrika Mashariki na Kati.
Azam ilianza kwa kushinda 1-0 dhidi ya KCCA, ikaichapa Al Malakia 2-0, ikimaliza hatua ya makundi kwa kuisambaratisha Adama City 5-0, katika robo fainali ikitoa Yanga kwa penalti 5-3, na nusu fainali ikaishinda KCCA 1-0 na fainali 2-0 dhidi ya Gor Mahia.
Kocha Stewart Hall akiwasifu wachezaji wake, hasa safu ya ulinzi kwa kucheza kwa umakini mkubwa muda wote wa mchezo.
“Tulicheza vizuri, ila mabeki walicheza vizuri zaidi na kuwazuia kabisa washambuliaji wao wasifi golini kwetu, kama ilivyokuwa katika michezo yote,” alisema Hall.
Azam ilianza mchezo kwa kasi katika dakika ya kwanza ilipata faulo iliyopigwa na Bocco lakini shuti lake lilitoka nje kidogo ya lango la Gor Mahia.
Azam iliendelea kulishambulia lango la Mahia wakitumia washambuliaji wake Tchetche, Bocco na Ame Ally waliokuwa mwiba kwa mabeki wa Wakenya hao.
Dakika ya 15, Tchetche aliwatoka mabeki wawili wa Gor Mahia na kupitisha krosi iliyomkuta Bocco aliyeusukimia mpira huo wavuni na kuamsha shangwe za mashabiki wa Azam ambao kabla ya bao hilo walionekana kuzidiwa na wenzao wa Mahia wakiongozwa na Raila Odinga. Bocco ndiye aliyefunga Azam bao la ushindi la kuipandisha timu hiyo daraja 2008 (dhidi ya Majimaji, Songea). Alifunga bao la kuipa ubingwa wa Ligi Kuu Bara kwa mara ya kwanza msimu wa 2012/13 (dhidi ya Mbeya City katika ushindi wa 2-1).
Pia, aliifungia bao la kwanza Azam FC katika mashindani ya mwaka huu ya Kombe la Kagame, na ndiye aliyefunga bao la kwanza la mchezo wa fainali dhidi ya Gor Mahia jana.
Gor Mahia ilikuwa na bahati ya pekee kumaliza mchezo huo wakiwa na wachezaji wote baada ya nyota wake Haruna Shakavu na Aucho Khalid kuwapiga viwango Himid Mao na Tchetche kwa nyakati tofauti, lakini mwamuzi Louis Hakizimana kutoka Rwanda alishindwa hata kutoa kadi za njano kwa wachezaji hao.
Baada ya matukio hayo Gor Mahia ilirudi mchezo na kuanza kufanya mashambulizi mfululizo langoni mwa Azam, lakini ukutu imara wa kipa Aishi Manula, na mabeki Pascal Wawa, Aggrey Morris ulifanya timu hiyo kwenda mapumziko ikiwa mbele kwa 1-0.
Wawa na Morris hawakumpa nafasi hata kidogo mshambuliaji Michael Olunga, hali iliyowafanya Gor Mahia kuanza kutumia krosi na kupiga mashuti ya mbali ambayo hayakuwa na madhara golini mwa Azam.
Azam ilianza kipindi cha pili kwa kumtoa Musa Farid, Ame Ally na kuwaingiza Erasto Nyoni na Frank Domayo kwa lengo la kuimarisha ulinzi na kutumia mipira mrefu kushambulia.
Tchetche nusura aipatie Azam bao la pili baada ya kupiga shuti lililomgonga begani kipa Oluoch na kurudi uwanjani kabla ya kuokolewa na mabeki wa Gor Mahia.
Azam ilipata bao la pili dakika 63, kwa mpira wa adhabu uliopigwa na Tchetche uliokwenda moja kwa moja wavuni na kumwacha kipa Olouch akijilaumu mwenyewe kwa uamuzi wake kudhani mpira huo unatoka nje.
Awali, KCCA ya Uganda ushindi wa tatu baada ya kuichapa Al Khartoum ya Sudan kwa mabao 2-1.
KCCA ilipata mabao yake kupitia Michael Birungi na Muzamir Mutyaba kabla ya Al Khartoum kupata bao la kufutia machozi kupitia Ousmaila Baba.