HALL AIKUBALI MUZIKI WA YANGA SC
Baada ya kuikosa Ngao Jamii kwa mara ya pili mfululizo mbele ya Yanga, Kocha Mkuu wa Azam FC, Muingereza Stewart Hall, amekiri kuwa vijana hao wa Mholanzi Hans van der Pluijm waliwazidi uwezo katika mechi hiyo iliyopigwa Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam juzi.
Hall pia alifafanua kuwa timu yake haikuwa vizuri katika dakika 20 za mwisho na walionekana wako tayari kusubiri kufika hatua ya matuta jambo ambalo halikuwa sahihi.
Kocha huyo alisema mechi hiyo ilikuwa ngumu na yenye ushindani kwa timu zote mbili hali iliyosababisha kumalizika dakika 90 za kawaida bila ya kufungana.
"Katika soka lazima uwe fiti kila upande, kama hauko fiti labda ukacheze mpira wa kikapu," alisema Hall.
Aliongeza kuwa mashabiki wa Yanga walisaidia pia kuipa ushindi timu yao, jambo lililowafanya wachezaji wao kujiona kama wako 12 kitu ambacho timu yake inakikosa.
"Nataka kusema jambo moja, mashabiki wa Yanga walifanya vizuri sana kuisaidia timu yao kwa kuishangilia, kitu ambacho sisi hatuna, kuna wakati unaona kama wako 12 uwanjani, au kama unacheza mechi nyingine, walikuwa wakiwashangilia kila walipokuwa na mpira na walituzomea pale tulipokuwa tunawashambulia," Hall aliongeza.
Pluijm alimjibu Hall kwa kueleza kuwa hiyo haikuwa sababu mojawapo ya yeye kufungwa kwa sababu kikosi chake kilikuwa pia kinashangiliwa na mashabiki wa Simba waliofika uwanjani hapo.
Mholanzi huyo alisema ushindi ambao timu yake iliupata juzi ni wa kulipa 'kisasi' na ulitokana na wachezaji wake kucheza katika kiwango cha juu ili kutimiza malengo yao.
Yanga ambao ni mabingwa watetezi wa Ligi Kuu ya Soka Tanzania Bara waliibuka na ubingwa wa Ngao ya Jamii baada ya kuifunga Azam kwa penalti 8-7 kufuatia timu hizo mbili kutoka suluhu ndani ya dakika 90 za kawaida.
Alisema mchezo huo ulikuwa mgumu na wenye ushindani lakini amefurahi timu yake ilifanikiwa kuibuka na ushindi na hatimaye kuanza vema msimu mpya wa ligi wa mwaka 2015/ 2016.
Pluijm alisema kila timu ilitengeneza mashambulizi kwa kiwango kinacholingana lakini akaipongeza zaidi safu yake ya ulinzi kwa kuwa makini ukilinganisha na mechi iliyopita.
"Katika soka kila siku kuna ushindani, na kila nafasi unayopata unatakiwa uitumie vizuri, tulitengeneza nafasi na wao walitengeneza nafasi pia, ulikuwa ni 50 kwa 50, hakuna ambaye alizidiwa moja kwa moja, hata ukiangalia kwenye mechi za Ligi Kuu ya England utashuhudia kuna baadhi ya mechi timu zinapanda na kushuka, ni hali ya kawaida kwenye mpira,"alisema kocha huyo ambaye timu yake iliondolewa na Azam katika hatua ya robo fainali kwenye mashindano ya Kombe la Kagame hivi karibuni.
Hata hivyo, Pluijm alisema kuwa kikosi chake hakikuwa kwenye kiwango cha juu katika dakika 90 za kawaida na kwamba hiyo ndiyo soka lakini amefurahishwa na ushindi walioupata ambao umewapa faraja.
Baada ya mechi hiyo, tayari msimu mpya umeanza na katika mechi ya ufunguzi Septemba 12, mwaka huu, Azam itaikaribisha Tanzania Prisons kwenye Uwanja wa Azam Complex, Chamazi jijini Dar es Salaam wakati Simba ikianzia ugenini Tanga kwa kuvaana na African Sports huku siku inayofuata Yanga yenyewe ikianza kutetea ubingwa wake kwa kucheza dhidi ya Coastal Union kutoka Tanga.