Ruka hadi kwenye maudhui makuu

HATA KAMA KUNA MACHAFUKO, NAKWENDA TU SAUZI- NGASSA

Winga wa Yanga ya jijini Dar es Salaam, Mrisho Ngasa, amesema kwamba licha ya hali ya machafuko inayoendelea nchini Afrika Kusini ya wazawa dhidi ya wageni, hatasita kwenda huko endapo atapokea mwaliko wa kujiunga na klabu yoyote  itakayomuhitaji.

Ngasa ambaye alirejea Yanga akitokea Simba kwa mkopo, anatarajia kumaliza mkataba wake Jangwani mwezi ujao.

Ngasa ambaye mwaka jana alikwenda Afrika Kusini kufanya majaribio 'kinyemela', anatajwa kuwa kwenye mipango ya kuhamia Free State Stars ya huko na ndio inayofanya achelewe kusaini mkataba mpya na Yanga.


Akizungumza jana jijini, Ngasa alisema kwamba yeye ni mchezaji na yuko tayari kwenda Afrika Kusini kujiunga na timu yoyote itakayoridhishwa na kiwango chake.

Mshambuliaji huyo ambaye juzi alifunga goli moja katika ushindi wa 3-2 dhidi ya Stand United, alisema kwamba soka ndio ajira yake hivyo anaamini kwamba akipata nafasi ya kwenda Afrika Kusini au nchi nyingine atakwenda kucheza mpira sehemu iliyo salama kwa sababu hatakuwa peke yake uwanjani.

"Mimi ni mwanajeshi, nitakwenda vitani wala sitaiachia fursa hiyo ikitokea, kiukweli wala sitahofia," alisema mshambuliaji huyo.

Alisema kwamba bado anaamini ana nafasi ya kwenda kucheza soka nje ya nchi na pia kuitumikia timu ya taifa (Taifa Stars) kwa muda mrefu.

Nyota huyo sasa amekuwa na ndoto za kucheza soka la kulipwa tofauti na mwaka 2012 alipokataa ofa ya kujiunga na El Merreikh ya Sudan iliyomuhitaji wakati huo akiwa anaichezea Azam.

Kutokana na Ngasa kukataa ofa ya El Merreikh na kuonyesha mapenzi yake kwa Yanga kwa kuibusu nembo ya klabu hiyo, Azam ilimtoa kwa mkopo Simba ambako aliitumikia kwa msimu mmoja.

Mbali na Ngasa, mchezaji mwingine wa Yanga aliye katika kikosi cha kwanza ambaye anamaliza mkataba mwezi ujao ni Mnyarwanda Haruna Niyonzima.

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

FIFA yatoa orodha ya vilabu bora duniani, Simba na Yanga zachuana vikali

SHIRIKISHO la Soka Afrika (CAF) limetoa orodha ya viwango vya ubora wa klabu barani, Simba ikiendelea kuwa juu ya klabu nyingine za Tanzania, nafasi ya tano. Orodha hiyo imetoka leo kuelekea droo ya hatua za awali za michuano ya klabu Afrika ambayo kwa mara ya kwanza kihistoria itafanyika nchini katika studio za Azam Tv, Tabata Jijini Dar es Salaam. Yanga ambayo kama Simba itashiriki Ligi ya Mabingwa — yenyewe inashika nafasi ya 12, wakati timu nyingine katika orodha hiyo ni Namungo FC wanaoshika nafasi ya mwisho, ya 75 kwa pamoja na Salitas FC ya Burkina Faso, Ahli Benghazi ya Libya na NAPSA Stars ya Zambia. Kwa msimu ujao mbali na Simba na Yanga kushiriki Ligi ya Mabingwa, Azam FC na Singida Black Stars zitashiriki michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika.

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

Timu inaitwa Mashujaa Lake Tanganyika FC ( Mashujaa FC ) ilianza rasmi kampeni yake ya kupanda Ligi Kuu tarehe 29/9/2018 na imepanda Ligi Kuu 25/06/2023 miaka mitano ya kupambana kwenye Ligi Daraja la kwanza Championship. Timu hii inaendeshwa kwa ushirikiano wa pande mbili kati ya Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) na Halmashauri ya Manispaa ya Kigoma Ujiji kwa niaba ya Wananchi wa Kigoma. Muelewe hapa maana wengi wanasema ni timu ya Jeshi asilimia 100% Nembo ya timu ni Sokwe Dume, Shujaa wa Hifadhi za Gombe na Mahale zilizopo mkoani Kigoma. Rangi ya kwanza ya jezi ya timu (first kit) ni hiyo hapo chini na kwenye nembo ya timu ni rangi za tunda la michikichi (mawese ). Hii kama njano ni mawese yaliyoganda na huo wekundu ni mawese ya moto. Ukishika tunda la Mse juu utaona wekundu na ukikata katikati utaona njano. Nyeupe ni ‘nazi’ ya Mse hizi ni alama za utajiri wa Kigoma Jezi nyingine ni blue inayowakilisha Ziwa Tanganyika na Jezi nyingine ni Nyeupe

Beno Ngassa mdogo wa Mrisho Ngassa anayekipiga Tanzania Prisons

Miongoni mwa viungo wa pembeni wanaofanya vizuri ni Benodict Khalfan Ngassa ambaye amekuwa akifanya vizuri. Ngassa ambaye ni mtoto wa mchezaji wa zamani wa Pamba Jiji na Simba SC, Khalfan Ngassa, pia ni mdogo wa kiungo mshambuliaji wa zamani wa Yanga, Simba na Azam, Mrisho Ngassa anatajwa ni mmoja kati ya wachezaji wanaotazamiwa kufanya makubwa siku za usoni. Mambo Uwanjani Blog itawaletea Makala maalum ya kiungo huyo hatari ambaye ndoto zake ni kufuata nyayo za kaka yake Mrisho Ngassa. Beno Ngassa