Di Maria kukosa mechi ya Liverpool
|
|
Mchezaji aliyenunuliwa pesa nyingi zaidi na
Manchester United Angel Di Maria atakosa mechi dhidi ya mahasimu hao wao
wa jadi Ligi ya Premia Jumapili lakini mzozo wa majeraha Old Trafford
kwa sasa unapungua, meneja Louis van Gaal alisema Ijumaa.
Winga huyo wa Argentina, aliyenunuliwa £59.7 milioni kutoka Real Madrid, ambayo ni rekodi Uingereza, atakosa mechi yake ya tatu mfululizo baada yake kukosa kupona jeraha la misuli ya paja.
Mabingwa hao mara 20 wa Uingereza pia watakuwa bila madifenda Luke Shaw na Chris Smalling waliojeruhiwa, sawa na kiungo wa kati Daley Blind.
vLakini meneja wa United Van Gaal alibaki mwenye matumaini Ijumaa, akisema mzozo wake wa majeraha utaisha karibuni. Mzozo huo ulikuwa umemkosesha raha mwanzo wa maisha yake Old Trafford, wakati mwingine akiwa bila wachezaji hadi 12 wakati mmoja.

"Sasa ni wachezaji wanne pekee wanaouguza majeraha, hivyo hali ni bora sasa,” Mholanzi huyo aliambia wanahabari.
United wamo nambari tatu kwenye jedwali na alama 28 kutoka kwa mechi 15, alama nane nyuma ya viongozi Chelsea, na wameshinda mechi tano zao za majuzi zaidi. Liverpool wamepitia kipindi kigumu tangu kuanza kwa msimu na wamo nambari tisa, alama saba nyuma ya vijana wa van Gaal.
Kocha huyo wa zamani wa Uholanzi atashuhudia uhasama mkali kati ya klabu hizo mbili kwa mara ya kwanza Jumapili, lakini ameomba ushauri kutoka kwa waliokaa sana klabu hiyo kuelewa vyema uhasama huo.
"Nina Ryan Giggs kama meneja msaidizi na aliwasilisha tathmini yake kuhusu Liverpool na alifanya hivyo vyema sana, nimependezwa sana,” van Gaal alisema kuhusu Giggs aliyechezea klabu hiyo mechi nyingi zaidi.
“Pia tuna mpishi na jina lake ni Mike na ninapokuwa sijui chochote kuhusu uhasama kati ya United na klabu nyingine yeye huniambia. Ni shabiki mkubwa wa Manchester United na kila mara hunijuza.”