LUHENDE AZUSHIWA ZENGWE MTIBWA.
Siku moja baada ya beki wa Mtibwa Sugar David Luhende kukosa penalti dhidi ya Simba, mashabiki wanaodhaniwa kuwa wa Mtibwa Sugar wamemshutumu beki huyo kwa kitendo chake cha kuinyima ushindi timu yao.
Wakizungumza kwa mtandao huu kwa njia ya simu, mashabiki hao wamemshutumu beki huyo kwa madai ya kuinyima ushindi Mtibwa ambao wameishia kutoka sare ya 1-1 na wekundu wa msimbazi.
Simba ilitangulia kupata bao ktk kipindi cha kwanza lililofungwa na Joseph Owino baada ya kupata pasi murua toka kwa Emmanuel Okwi.
Kabla ya kuelekea mapumziko Mtibwa Sugar walipata penalti iliyokwenda kupigwa na David Luhende ambapo iliokolewa na mlinda mlango chipukizi Peter Manyika Jr.
Manyika alitumia udhaifu wa Luhende kwa kumsoma miguu yake wakati akijiandaa kupiga. Hata hivyo Luhende alikosa penalti hiyo baada ya kipa kuiokoa, Mtibwa walichomoa bao hilo ktk kipindi cha pili likifungwa na Mussa Hassan Mgosi.
Ktk mchezo huo Luhende alishindwa kung'ara hivyo mashabiki wa Mtibwa walianza kumshutuma kiasi kwamba kocha wa timu hiyo Mecky Mexime aliamua kumtoa