Ruka hadi kwenye maudhui makuu

UHURU SELEMAN ARUDISHWA SIMBA.

WINGA Uhuru Suleiman Mwambungu ameamua kurejea klabu yake ya Simba SC kumalizia Mkataba wake wa miezi saba kutoka Coastal Union ya Tanga alikopelekwa kwa mkopo mwanzoni mwa msimu.

Uhuru aliyekwenda Coastal akitokea Azam FC alikocheza pia kwa mkopo kwa nusu msimu, amesema jana usiku kwamba tayari amekwishafuata taratibu za kumrejesha klabu yake.

Amesema amekwishauarifu uongozi wa Coastal ambao umeandika barua ya kumrejesha Simba SC baada ya kuitumikia vizuri klabu hiyo katika mzunguko wa kwanza wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara msimu huu.

“Kama utakumbuka nilitolewa kwa mkopo Simba SC kwenda Azam FC Desemba mwaka jana kwa sababu sikuwa fiti, nilikuwa nimetoka kwenye maumivu.

Lakini namshukuru Mungu nimefika Azam nimepata malezi mazuri na nimecheza kidogo hadi nimefanikiwa kuwa fiti,”.


“Mwanzoni mwa msimu nimekwenda Coastal, huko kwa kweli ndiyo mambo yamekuwa mazuri zaidi, nimepata nafasi ya kutosha, nimecheza hadi sasa najiona kabisa nimerudi katika kiwango changu, hiyo ni kwa mtu yeyote aliyeniona anaweza kuthibitisha hilo,”alisema.

Uhuru alisema kwamba umewadia wakati sasa wa yeye kulipa fadhila kwa Simba SC baada ya kumgharimia matibabu ya goti nchini India mwaka juzi alipoumia na kukaa nje ya Uwanja kwa msimu mzima.

“Tangu nimepona kwa kweli sijapata fursa ya kulipa fadhila kwa Simba SC, na ninaamini huu ni wakati mwafaka sasa kuwalipa fadhila Simba SC na nimeamua kurudi klabu yangu, kurudi nyumbani kuisaidia timu yangu,”alisema.

Uhuru pia amesema amekwishafanya mazungumzo na Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Simba SC, Zacharia Hans Poppe ambaye ameafiki suala hilo na anatarajia mazoezi yatakapoanza atajiunga na wenzake.

Baada ya kuteswa na maumivu kwa miaka miwili, hatimaye Uhuru alionyesha amerejea katika kiwango chake katika mzunguko wa kwanza wa Ligi Kuu, akiichezea Coastal Union.

Pamoja na ujuzi wake, lakini uzoefu wa Uhuru ni kitu ambacho kinatarajiwa kuisaidia sana Smba SC iwapo atasajiliwa katika mzunguko wa pili wa Ligi Kuu.

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

FIFA yatoa orodha ya vilabu bora duniani, Simba na Yanga zachuana vikali

SHIRIKISHO la Soka Afrika (CAF) limetoa orodha ya viwango vya ubora wa klabu barani, Simba ikiendelea kuwa juu ya klabu nyingine za Tanzania, nafasi ya tano. Orodha hiyo imetoka leo kuelekea droo ya hatua za awali za michuano ya klabu Afrika ambayo kwa mara ya kwanza kihistoria itafanyika nchini katika studio za Azam Tv, Tabata Jijini Dar es Salaam. Yanga ambayo kama Simba itashiriki Ligi ya Mabingwa — yenyewe inashika nafasi ya 12, wakati timu nyingine katika orodha hiyo ni Namungo FC wanaoshika nafasi ya mwisho, ya 75 kwa pamoja na Salitas FC ya Burkina Faso, Ahli Benghazi ya Libya na NAPSA Stars ya Zambia. Kwa msimu ujao mbali na Simba na Yanga kushiriki Ligi ya Mabingwa, Azam FC na Singida Black Stars zitashiriki michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika.

Beno Ngassa mdogo wa Mrisho Ngassa anayekipiga Tanzania Prisons

Miongoni mwa viungo wa pembeni wanaofanya vizuri ni Benodict Khalfan Ngassa ambaye amekuwa akifanya vizuri. Ngassa ambaye ni mtoto wa mchezaji wa zamani wa Pamba Jiji na Simba SC, Khalfan Ngassa, pia ni mdogo wa kiungo mshambuliaji wa zamani wa Yanga, Simba na Azam, Mrisho Ngassa anatajwa ni mmoja kati ya wachezaji wanaotazamiwa kufanya makubwa siku za usoni. Mambo Uwanjani Blog itawaletea Makala maalum ya kiungo huyo hatari ambaye ndoto zake ni kufuata nyayo za kaka yake Mrisho Ngassa. Beno Ngassa

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

Timu inaitwa Mashujaa Lake Tanganyika FC ( Mashujaa FC ) ilianza rasmi kampeni yake ya kupanda Ligi Kuu tarehe 29/9/2018 na imepanda Ligi Kuu 25/06/2023 miaka mitano ya kupambana kwenye Ligi Daraja la kwanza Championship. Timu hii inaendeshwa kwa ushirikiano wa pande mbili kati ya Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) na Halmashauri ya Manispaa ya Kigoma Ujiji kwa niaba ya Wananchi wa Kigoma. Muelewe hapa maana wengi wanasema ni timu ya Jeshi asilimia 100% Nembo ya timu ni Sokwe Dume, Shujaa wa Hifadhi za Gombe na Mahale zilizopo mkoani Kigoma. Rangi ya kwanza ya jezi ya timu (first kit) ni hiyo hapo chini na kwenye nembo ya timu ni rangi za tunda la michikichi (mawese ). Hii kama njano ni mawese yaliyoganda na huo wekundu ni mawese ya moto. Ukishika tunda la Mse juu utaona wekundu na ukikata katikati utaona njano. Nyeupe ni ‘nazi’ ya Mse hizi ni alama za utajiri wa Kigoma Jezi nyingine ni blue inayowakilisha Ziwa Tanganyika na Jezi nyingine ni Nyeupe