Ruka hadi kwenye maudhui makuu

AL AHLY MABINGWA AFRIKA.

Klabu ya Al Ahly ya Misri imeshinda taji la klabu bingwa Afrika ilipoicharaza Orlando Pirates ya Afrika Kusini kwa mabao 2-0 katika mkondo wa pili na wa mechi ya mwisho mjini Cairo Jumapili.

Ahly, waliojinyakulia kombe hilo kwa mara ya saba walipata alama 3-1 kwa ujumla.

Kulikuwa na ripoti za vurugu kuzuka kati ya mamia ya wafuasi wa Ahly na polisi nchini Misri, kabla ya mchuano kuanza.

Pindi vurugu zilipositishwa , mchezaji gwiji, Mohamed Aboutrika ndiye aliyeingiza bao la kwanza katika dakika ya 54. Ahmed Abdul Zaher aliingiza bao la pili kwa Ahly katika dakika 78.

Hata hivyo mabingwa wa Misri walipungua kwa mtu mmoja na kusalia 10 dakika sita baada ya difenda Sherif Abdel Fadil kuondolewa uwanjani kwa kumfanyia masihara Daine Klate.


Pirates, waliibuka mabingwa mwaka mwaka 1995, walicheza kadri ya uwezo wao, lakini waliondokewa na matumaini Ahly walipoingiza bao lao la pili katika uwanja uliokuwa umesongamana watu mjini Cairo.

Hata hivyo mabingwa hao wa Afrika Kusini walikosa nafasi kadhaa za kuingiza bao.

Ahly wamepata kombe hilo pamoja na kitita cha dola milioni moja na nusu

Pia watawakilisha Afrika katika kombe la dunia la klabu bingwa duniani litakalofanyika nchini Morocco mwezi ujao.

Mamia ya mashabiki wa Ahly walikabiliana na polisi kabla ya mechi kuong’oa nanga. Ni mechi ya kwanza kubwa ambako mashabiki wameruhusiwa kuingia uwanjani tangu watu 74 wengi waliokuwa mashabiki wa Al Ahly , waliuawa katika mechi iliyokumbwa na vurugu mwaka jana.

Polisi wlailazimika kutumia gesi ya kutoa machozi, kuwatawanya mashabiki waliokuwa wanatupia mawe huku wakiingia kwa lazima ndani ya uwanja.

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

FIFA yatoa orodha ya vilabu bora duniani, Simba na Yanga zachuana vikali

SHIRIKISHO la Soka Afrika (CAF) limetoa orodha ya viwango vya ubora wa klabu barani, Simba ikiendelea kuwa juu ya klabu nyingine za Tanzania, nafasi ya tano. Orodha hiyo imetoka leo kuelekea droo ya hatua za awali za michuano ya klabu Afrika ambayo kwa mara ya kwanza kihistoria itafanyika nchini katika studio za Azam Tv, Tabata Jijini Dar es Salaam. Yanga ambayo kama Simba itashiriki Ligi ya Mabingwa — yenyewe inashika nafasi ya 12, wakati timu nyingine katika orodha hiyo ni Namungo FC wanaoshika nafasi ya mwisho, ya 75 kwa pamoja na Salitas FC ya Burkina Faso, Ahli Benghazi ya Libya na NAPSA Stars ya Zambia. Kwa msimu ujao mbali na Simba na Yanga kushiriki Ligi ya Mabingwa, Azam FC na Singida Black Stars zitashiriki michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika.

Beno Ngassa mdogo wa Mrisho Ngassa anayekipiga Tanzania Prisons

Miongoni mwa viungo wa pembeni wanaofanya vizuri ni Benodict Khalfan Ngassa ambaye amekuwa akifanya vizuri. Ngassa ambaye ni mtoto wa mchezaji wa zamani wa Pamba Jiji na Simba SC, Khalfan Ngassa, pia ni mdogo wa kiungo mshambuliaji wa zamani wa Yanga, Simba na Azam, Mrisho Ngassa anatajwa ni mmoja kati ya wachezaji wanaotazamiwa kufanya makubwa siku za usoni. Mambo Uwanjani Blog itawaletea Makala maalum ya kiungo huyo hatari ambaye ndoto zake ni kufuata nyayo za kaka yake Mrisho Ngassa. Beno Ngassa

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

Timu inaitwa Mashujaa Lake Tanganyika FC ( Mashujaa FC ) ilianza rasmi kampeni yake ya kupanda Ligi Kuu tarehe 29/9/2018 na imepanda Ligi Kuu 25/06/2023 miaka mitano ya kupambana kwenye Ligi Daraja la kwanza Championship. Timu hii inaendeshwa kwa ushirikiano wa pande mbili kati ya Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) na Halmashauri ya Manispaa ya Kigoma Ujiji kwa niaba ya Wananchi wa Kigoma. Muelewe hapa maana wengi wanasema ni timu ya Jeshi asilimia 100% Nembo ya timu ni Sokwe Dume, Shujaa wa Hifadhi za Gombe na Mahale zilizopo mkoani Kigoma. Rangi ya kwanza ya jezi ya timu (first kit) ni hiyo hapo chini na kwenye nembo ya timu ni rangi za tunda la michikichi (mawese ). Hii kama njano ni mawese yaliyoganda na huo wekundu ni mawese ya moto. Ukishika tunda la Mse juu utaona wekundu na ukikata katikati utaona njano. Nyeupe ni ‘nazi’ ya Mse hizi ni alama za utajiri wa Kigoma Jezi nyingine ni blue inayowakilisha Ziwa Tanganyika na Jezi nyingine ni Nyeupe