TAMBWE, KAZE SASA KUKIPIGA SIMBA, MOTO WAO UTAWAKA DHIDI YA OLJORO
Hatimaye wachezaji wapya wa Simba kutoka Burundi mshambuliaji Amisi Tambwe na beki Gilbert Kaze (Pihani) kutoka Burundi, jana walipata uhamisho wa kimataifa kwa ajili ya kuanza kuichezea klabu hiyo inayoshiriki Ligi Kuu ya Soka Tanzania Bara, ilielezwa jijini Dar es Salaam jana.
Tambwe na Kaze juzi Jumamosi walishindwa kuitumikia timu yao hiyo kutokana na kukosa ITC na kusababisha mwenyekiti wa Simba, Ismail Aden Rage, juzi asafiri kwenda Burundi kukamilisha usajili wa wachezaji hao.
Tambwe na Kaze waliwasili nchini wiki iliyopita na siku iliyofuata walielekea Kahama, Shinyanga kuungana na wachezaji wengine wa Simba ambao walikuwa wameweka kambi mkoani humo kujiandaa na msimu mpya wa ligi ulioanza Jumamosi.
Akizungumza na mtandao huu, Katibu Mkuu wa Simba, Evodius Mtawala, alisema kuwa tayari wamekamilisha uhamisho wa wachezaji hao na keshokutwa Jumatano watashuka uwanjani kuitumikia timu hiyo kwa mara ya kwanza watakapoivaa JKT Oljoro kwenye uwanja wa Sheikh Amri Abeid jijini Arusha.
"Tumekamilisha mchana huu (jana mchana), Jumatano watacheza, tunashukuru tumewapata," alisema Mtawala.
Alieleza kwamba usajili huo umefanikishwa na safari ya mwenyekiti, Ismail Aden Rage, ambaye juzi alilazimika kusafiri hadi Burundi kwenda kukamilisha usajili huo kufuatia 'siasa' kuanza kuingia baada ya nchi hiyo kuona kwamba itawakosa wachezaji hao katika mechi za mashindano ya Kombe la Mataifa ya Afrika kwa wachezaji wa ndani (CHAN) zitakazofanyika mapema mwakani.
Aliongeza kuwa suala la Betram Mwombeki na klabu yake ya zamani ya Pamba ya jijini Mwanza pia limefanyiwa kazi kwa kuwapa Sh. milioni mbili ili kubariki uhamisho huo.
Aliwataka mashabiki wa Simba kuwa na utulivu na matokeo mazuri yatapatikana katika timu yao.
Simba ilianza kwa sare ya magoli 2-2 dhidi ya Rhino Rangers ambayo imepanda daraja na kucheza Ligi Kuu kwa mara ya kwanza tangu ilipoanzishwa.