TAMBWE AANZA MCHECHETO LIGI KUU, ADAI NI NGUMU KULIKO KWAO BURUNDI
Baada ya kucheza kwa mara ya kwanza katika Ligi Kuu ya Tanzania Bara, mshambuliaji Amisi Tambwe (Pichani) wa Simba amesema ligi hiyo ni ngumu ukilinganisha na Ligi Kuu ya Burundi aliyotokea.
Tambwe, mfungaji bora michuano ya Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati (Kombe la Kagame) mwaka huu, ametua Simba akitokea Vital'O inayoshiriki Ligi Kuu ya Burundi. Akizungumza jana asubuhi kwenye hoteli ambayo Simba walikuwa wamefikia jijini hapa, Tambwe alisema alishindwa kuziona nyavu katika mechi yao ya juzi dhidi ya Oljoro kwa sababu alikumbana na vikwazo vingi uwanjani.
"Kwa kweli ligi ya Tanzania ni ngumu kuliko ya kwetu (Burundi). Timu zinakamia sana. Nilifanya kila mbinu ili nifunge lakini uwanja ulikuwa tatizo.
Haikuwa rahisi kukimbia huku ukimiliki mpira," alisema Tambwe. "Wapinzani wetu walikuwa wametukamia ndiyo maana ilibidi nicheze kwa tahadhari nikihofu kuvunjwa viungo. "Tunashukuru Mungu kwa kupata ushindi na mashabiki wetu watusamehe kwa kupoteza nafasi nyingi.
"Mechi ya jana karibu kila kitu kilikuwa kigeni kwangu - uwanja, mfumo wa Simba na hata wachezaji wa timu yetu.
Ukiwaondoa Chollo, Kiemba na Kaze, wengine wapya ni kwangu. Nahitaji muda kuwasoma."
Baada ya kumalizika kwa michuano ya Kombe la Kagame ambayo mwaka huu ilifanyika Sudan, Tambwe na Mrundi mwenzake beki Gilbert Kaze walisaini mikataba ya miaka miwili kuitumikia Simba.
Wawili hao, ambao pia ni wachezaji tegemeo katika timu ya taifa ya Burundi, walitoa mchango mkubwa katika klabu ya Vital'O waliyoipa ubingwa wa Kombe la Kagame Julai.
Kaze na Tambwe pia wamesaidia kuivusha Burundi kushiriki Fainali za Afrika kwa Wachezaji wa Ndani (CHAN), nafasi ambazo wawili hao tayari wamejivua ushiriki baada ya kusaini kuichezea Simba ambayo iko nje ya nchi yao.
Hadi anatua Simba wiki iliyopita, Tambwe alikuwa anaongoza safu ya wafungaji wa ligi kuu ya Burundi akiifungia Vital'O magoli 21 katika mechi 18 msimu huu.