WALIOTEMWA SIMBA WAIBUKIA MTIBWA SUGAR
Mshambuliaji aliyeshindwa kupata namba katika kikosi
cha kwanza cha Simba msimu uliopita Abdallah Juma (Pichani), amejiunga na timu ya Mtibwa Sugar inayoshiriki ligi kuu ya Bara ijayo pamoja na beki
Paul Ngalema ambaye wamejiunga naye wote kwenye timu hiyo.
Nyota hao waliachwa na Simba baada ya kumalizika kwa msimu wa ligi kuu uliopita kwa madai ya kushuka kwa uwezo wao lakini sasa wataichezea Mtibwa kuanzia msimu ujao.
Akizungumza jana, kocha wa Mtibwa Sugar, Meck Mexime alisema wamewasajili wachezaji hao ili kuziba mapengo ya baadhi ya nyota wake walioiacha timu hiyo na kwenda kujiunga na klabu za Simba na Yanga.
Mbali na Juma na Ngalema ambao wamesaini mkataba wa miaka miwili wa kuitumikia timu hiyo, Mtibwa imesajili aliyekuwa golikipa namba mbili wa mabingwa wa Bara Yanga, Said Mohamed.
Wachezaji hao kwa pamoja hivi sasa wapo na kikosi cha timu hiyo kilichopiga kambi jijini Dar es Salaam kwa maandalizi ya michuano hiyo inayotarajiwa kuanza Agosti 24.
Mexime alisema wamemsajili Ngalema ili kuziba pengo la Issa Rashid aliyejiunga na Simba na Juma ambaye Mtibwa ilimuuza kwa Simba mwaka jana, amesajiliwa kuziba nafasi ya Hussen Javu ambaye wiki hii amekamilisha kujiunga na Yanga.
"Said Mohamed yeye tumemsajili ili kuimarisha safu yetu ya ulinzi ili asaidiane na magolikipa waliopo sasa," alisema Maxime.
Aidha, alisema kuwa wanaamini usajili huo utainua viwango vya wachezaji hao amabao wameonekana hawafai walikotoka.
"Tunaamini katika usajili huu, msimu ujao timu zilizowaacha zitakuja tena na kutaka kuwasajili kwa sababu uwezo wao utakua na wataonekana tena bora," alisema Maxime ambaye ni nahodha wa zamani na wa muda mrefu wa Mtibwa na timu ya taifa, Taifa Stars.
Wakati huo huo Mtibwa Sugar itapambana na Yanga katika mchezo wa kirafiki utakaofanyika kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam Jumatano.