VALENCIA YAMPANDIA DAU CHICHARITO, MAN U WAINGIA MCHECHETO
KLABU ya Valencia inamtaka mshambuliaji wa Manchester United, Javier Hernandez maarufu kama Chicharito (Pichani) kwa mkopo.
Klabu hiyo ya Hispania imeandaa orodha
fupi kusaka mchezaji wa kuziba pengo la Roberto Soldado ambaye
anakaribia kujiunga na Tottenham, lakini pia anatakiwa na Liverpool.
Valencia imeweka bajeti maalum na hiyo inahusisha pia mshambuliaji kinda wa Manchester City,John Guidetti.
Anatakiwa: Valencia inamtaka Javier Hernandez ahamie Hispania kuziba pengo la mshambuliaji wake anayetaka kuondoka
Anaondoka: Roberto Soldado anatakiwa na Tottenham na Liverpool
Pamoja na hayo, wanaamini wanaweza
kumpata Hernandez kwa sababu kwa sasa hana namba ya kudumu katika kikosi
cha kwanza cha Mashetani Wekundu.
Mshambuliaji huyo wa Mexico amekuwa
hatumiki sana kwa miezi 18 iliyopita, kufuatia kuwasili kwa Robin van
Persie. Pia amekuwa akijadiliwa na Atletico Madrid na Juventus katika
miezi ya karibuni, lakini amerudia kusema anataka kubaki Old Trafford.
Kocha David Moyes ni shabiki mkubwa wa
mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 23 na haitakuwa rahisi kumruhusu
kuondoka, hususan kutokana na kwamba United bado haijasajili mchezaji
mwenye jina kubwa inamyemtaka.
Mustakabali wa Wayne Rooney pia
unachangia, United inapambana kumzuia mshambuliaji huyo wa kimataifa wa
England kumzuia kuhamia kwa wapinzani Chelsea na Arsenal.
Shabiki mkubwa: David Moyes anampenda Hernandez na haitakuwa rahisi kumruhusu kuondoka