STARS YAAPA KUIGALAGAZA UGANDA KESHO
Nahodha wa timu ya soka ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars) (Pichani), Juma Kaseja,
amesema wamejiandaa kubadili matokeo kwa kushinda dhidi ya wenyeji
Uganda (The Cranes) katika mechi ya marudiano ya kuwania kufuzu kwa
fainali zijazo za Kombe la Mataifa ya Afrika kwa wachezaji wa ligi za
ndani (CHAN) na hivyo kutibua rekodi ya wenyeji ya kutowahi kufungwa
nyumbani katika mechi yoyote ya michuano tangu mwaka 2005.
Stars walitua salama nchini Uganda juzi na kuanza maandalizi yao ya mwisho kabla ya kuteremka dimbani kesho kuwakabili wenyeji kwenye Uwanja wa Mandela uliopo jijini Kampala kuanzia saa 10:00 jioni.
Stars iliyolala kwa goli 1-0 katika mechi yao ya kwanza iliyochezwa Julai 13 jijini Dar es Salaam, ina kibarua kizito kesho kwani itatakiwa kushinda walau 2-0 ili kusonga mbele.
Hata hivyo, Kaseja na wenzake wanaamini kuwa wanao uwezo wa kushinda kesho na kuvunja rekodi nzuri ya Cranes kutofungwa kwenye ardhi yao ya nyumbani tangu mwaka 2005.
Akizungumza na mtandao huu kutokea jijini Kampala jana, Kaseja alisema wachezaji wote kikosini wako ‘fiti’ na wamepania kucheza kufa au kupona kwa nia ya kuibuka na ushindi, hasa baada ya kuwafahamu vyema wapinzani wao kulinganisha na vile ilivyokuwa katika mechi ya kwanza wiki mbili zilizopita.
Kaseja alisema pia wapinzani wao watacheza wakiwa na hofu ya kuwatuliza mashabiki wao ambao wana kiu ya kuona kikosi hicho kinafuzu kushiriki fainali hizo kwa mara ya kwanza.
"Tuko vizuri na tutaweza kubadili ubao wa matokeo. Ni zamu yetu sasa kushinda ugenini kama wao walivyotufunga nyumbani kwetu," alisema Kaseja, akiongeza kuwa salamu za kheri walizopata kutoka kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jakaya Kikwete, zimewaongezea morali ya kuibuka na ushindi.
KOCHA POULSEN
Katika hatua nyingine, kocha wa Stars, Kim Poulsen alisema ingawa mechi hiyo ni ngumu, lakini kikosi chake kimejiandaa kuikabili Uganda kwani wachezaji wako wako vizuri na ari kwa ajili ya mechi.
Alisema wachezaji wote wako katika hali nzuri, isipokuwa Khamis Mcha aliyekuwa na maumivu ya goti, lakini kwa mujibu wa madaktari wa timu anaendelea vizuri kwani tayari wanampa mazoezi mepesi.
Kikosi cha kamili cha Stars kilichotua Kampala jana kinaundwa na makipa Juma Kaseja, Mwadini Ali na Ali Mustafa. Mabeki ni Aggrey Morris, David Luhende, Erasto Nyoni, Kelvin Yondani, Nadir Haroub na Vincent Barnabas. Viungo ni Amri Kiemba, Athuman Idd, Frank Domayo, Haruni Chanongo, Khamis Mcha, Mudhathir Yahya, Salum Abubakar na Simon Msuva. Washambuliaji ni John Boko, Juma Luizio na Mrisho Ngasa.
Wakati huo huo, Kocha Kim Poulsen atakuwa na mkutano na waandishi wa habari siku ya Jumatatu (Julai 29 mwaka huu). Mkutano huo utafanyika saa 5 kamili asubuhi katika ukumbi wa mikutano wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF).