Ruka hadi kwenye maudhui makuu

MAN UNITED YANUSURIKA KICHAPO



Bao la dakika za lala salama kutoka kwa Wilfried Zaha liliokoa Manchester United kutoka kwa kichapo cha aibu cha tatu katika ziara yao ya kipindi cha kabla ya msimu bara Asia mnamo Ijumaa, na kutoka sare 2-2 na Cerezo Osaka timu aliyochezea Shinji Kagawa katika Ligi-J.

Kagawa, aliyehamia Old Trafford kutoka Borussia Dortmund mwaka mmoja uliopita, pia alisisimua mashabiki 44,856 waliofurika uwanja wa Nagai kwa kufungia United bao lake la kwanza baao ya kupoteza penalti kwa kupiga mkwaju moja kwa moja hadi mikononi mwa kipa wa Osaka Kim Jin-Hyeon.
Red Devils sasa wameshinda mechi mbili na kushindwa mbili Asia baada ya kupoteza 1-0 mikononi mwa timu ya All Stars wa Ligi ya Thailand wiki mbili zilizopita mjini Bangkok, wakawalemea All Stars wa Ligi A mjini Sydney na tena wakawainamia Yokohama Marinos wa Ligi J Jumane iliyopita.
Straika wa Cerezo Kenyu Sugimoto alifungua ukurasa wa mabao kunako dakika ya 34 kwa kuwachenga walinzi wawili na kutoa kombora kwa guu la kushoto ambalo lilimpita Lindegaard baada ya kunasa pasi iliyokuwa imetolewa na Chris Smalling wa United.
United nusura wasawazishe dakika ya 40 pale Kagawa alipotoa kombora la juu baada ya straika Mholanzi Robin van Persie kumwandalia mpira maridadi alioupata kutoka kwa mpira uliodunda kutoka kwa kombora la Danny Welback mlingoti wa kushoto.
Kagawa alipoteza penalti dakika ya 53 pale Ashley Young alipochezewa visivyo eneo la hatari na difenda wa Cerezo Tatsuya Yamashita.
Lakini Mjapani huyo wa umri wa miaka 24 alijirejeshea hadhi yake kwa kufunga dakika mbili baadaye, kwa kutuma mpira wavuni kupitia katikati ya miguu ya Kim baada ya kupata mpira ulioandaliwa na Ryan Giggs.
Dakika chache baadaye, Kagawa alitolewa uwanjani huku akishangiliwa na mashabiki wake wa zamani, na muda si muda Cerezo wakawashangaza mabingwa hao wa Uingereza kwa bao la pili kupitia mshambuliaji wa umri wa miaka 18 Takumi Minamino dakika ya 63.
Kombora la Minamino kutoka upande wa kushoto nje ya eneo la hatari lilielekea juu ndani ya wavu. Lakini Zaha aliwaliwaza wageni na kuwaokoa kutoka kwa aibu kwa kufunga bao la kusawazisha dakika moja kabla ya mechi kumalizika baada ya kupata mpira ulioandaliwa na Jesse Lingard.
Katika mechi yao ya mwisho ziara yao ya Asia, mabingwa hao wa Uingereza watacheza dhidi Kitchee FC mjini Hong Kong mnamo Jumatatu na kuhitimisha kampeni yao ya kabla ya msimu kwa mechi ya kirafiki dhidi ya AIK Fotboll ya Sweden mjini Stockholm Agosti 6.
United chini ya David Moyers – aliyeteuliwa mrithi wa kocha wa muda mrefu Alex Ferguson mwishoni mwa msimu uliopita – ataanza kampeni yake ya kutetea taji dhidi ya Swansea City ugenini Agosti 17.

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

FIFA yatoa orodha ya vilabu bora duniani, Simba na Yanga zachuana vikali

SHIRIKISHO la Soka Afrika (CAF) limetoa orodha ya viwango vya ubora wa klabu barani, Simba ikiendelea kuwa juu ya klabu nyingine za Tanzania, nafasi ya tano. Orodha hiyo imetoka leo kuelekea droo ya hatua za awali za michuano ya klabu Afrika ambayo kwa mara ya kwanza kihistoria itafanyika nchini katika studio za Azam Tv, Tabata Jijini Dar es Salaam. Yanga ambayo kama Simba itashiriki Ligi ya Mabingwa — yenyewe inashika nafasi ya 12, wakati timu nyingine katika orodha hiyo ni Namungo FC wanaoshika nafasi ya mwisho, ya 75 kwa pamoja na Salitas FC ya Burkina Faso, Ahli Benghazi ya Libya na NAPSA Stars ya Zambia. Kwa msimu ujao mbali na Simba na Yanga kushiriki Ligi ya Mabingwa, Azam FC na Singida Black Stars zitashiriki michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika.

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

Timu inaitwa Mashujaa Lake Tanganyika FC ( Mashujaa FC ) ilianza rasmi kampeni yake ya kupanda Ligi Kuu tarehe 29/9/2018 na imepanda Ligi Kuu 25/06/2023 miaka mitano ya kupambana kwenye Ligi Daraja la kwanza Championship. Timu hii inaendeshwa kwa ushirikiano wa pande mbili kati ya Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) na Halmashauri ya Manispaa ya Kigoma Ujiji kwa niaba ya Wananchi wa Kigoma. Muelewe hapa maana wengi wanasema ni timu ya Jeshi asilimia 100% Nembo ya timu ni Sokwe Dume, Shujaa wa Hifadhi za Gombe na Mahale zilizopo mkoani Kigoma. Rangi ya kwanza ya jezi ya timu (first kit) ni hiyo hapo chini na kwenye nembo ya timu ni rangi za tunda la michikichi (mawese ). Hii kama njano ni mawese yaliyoganda na huo wekundu ni mawese ya moto. Ukishika tunda la Mse juu utaona wekundu na ukikata katikati utaona njano. Nyeupe ni ‘nazi’ ya Mse hizi ni alama za utajiri wa Kigoma Jezi nyingine ni blue inayowakilisha Ziwa Tanganyika na Jezi nyingine ni Nyeupe

Beno Ngassa mdogo wa Mrisho Ngassa anayekipiga Tanzania Prisons

Miongoni mwa viungo wa pembeni wanaofanya vizuri ni Benodict Khalfan Ngassa ambaye amekuwa akifanya vizuri. Ngassa ambaye ni mtoto wa mchezaji wa zamani wa Pamba Jiji na Simba SC, Khalfan Ngassa, pia ni mdogo wa kiungo mshambuliaji wa zamani wa Yanga, Simba na Azam, Mrisho Ngassa anatajwa ni mmoja kati ya wachezaji wanaotazamiwa kufanya makubwa siku za usoni. Mambo Uwanjani Blog itawaletea Makala maalum ya kiungo huyo hatari ambaye ndoto zake ni kufuata nyayo za kaka yake Mrisho Ngassa. Beno Ngassa