Ruka hadi kwenye maudhui makuu

GARETH BALE AKOSA KUWEKA REKODI YA DUNIA

Bale out: Will Welsh wizard been seen again in Tottenham shirt?NYOTA wa Tottenham, Gareth Bale amekasirika baada ya klabu yake kupiga chini ofa ya kuvunja rekodi ya dunia ya usajili kwa ajili yake Pauni Milioni 82 kutoka Real Madrid.


Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 24 hakuwepo kwenye mechi ya kujiandaa na msimu ya klabu yake mjini Hong Kong jana- na hajisikii kuendelea kuvaa jezi nyeupe za Tottenham tena.

Kocha Andre Villas Boas aliamua kutomjumiisha nyota huyo wa Wales katika michuano ya wiki hii Barclays Asia Trophy kutokana na matatizo ya misuli. Lakini ukweli ni kwamba, mchezaji huyo yuko fiti kucheza- lakini wamemvuruga.

Alielekeza moyo wake kwenda Madrid kucheza Ligi ya Mabingwa sambamba na nyota wa soka akina Cristiano Ronaldo, Mesut Ozil, Luka Modric na Karim Benzema.

Lakini uamuzi wa mwisho juu ya ndoto zake za kuondoka upo kwa Mwenyekiti wa Spurs, Daniel Levy, ambaye amekuwa akihakikisha Bale anamalizia Mkataba wake wa miaka mitatu.

Na kutokana na Wales kukosa nafasi ya kufuzu katika Fainali zijazo za Kombe la Dunia, Bale anaona ni vyema ajakaribu bahati yake katika michuano mikubwa Ulaya na akiwa anaelekea kutimiza miaka 25, katika kipindi chote alichocheza soka, amecheza hatua hiyo ya michuano mara moja tu.

Ikicheza bila Bale, Spurs iliifunga China Kusini mabao 6-0 katika mechi iliyochezwa kwenye mvua Hong Kong. Mechi ijayo ya kirafiki ya Tottenham ni dhidi ya Monaco Jumamosi na Villas Boas amesema: "Kuna uwezekano mkubwa yeye (Bale) atakuwa fiti. Atakuwa fiti kujiunga na timu kwa mazoezi Jumatano,".

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

FIFA yatoa orodha ya vilabu bora duniani, Simba na Yanga zachuana vikali

SHIRIKISHO la Soka Afrika (CAF) limetoa orodha ya viwango vya ubora wa klabu barani, Simba ikiendelea kuwa juu ya klabu nyingine za Tanzania, nafasi ya tano. Orodha hiyo imetoka leo kuelekea droo ya hatua za awali za michuano ya klabu Afrika ambayo kwa mara ya kwanza kihistoria itafanyika nchini katika studio za Azam Tv, Tabata Jijini Dar es Salaam. Yanga ambayo kama Simba itashiriki Ligi ya Mabingwa — yenyewe inashika nafasi ya 12, wakati timu nyingine katika orodha hiyo ni Namungo FC wanaoshika nafasi ya mwisho, ya 75 kwa pamoja na Salitas FC ya Burkina Faso, Ahli Benghazi ya Libya na NAPSA Stars ya Zambia. Kwa msimu ujao mbali na Simba na Yanga kushiriki Ligi ya Mabingwa, Azam FC na Singida Black Stars zitashiriki michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika.

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

Timu inaitwa Mashujaa Lake Tanganyika FC ( Mashujaa FC ) ilianza rasmi kampeni yake ya kupanda Ligi Kuu tarehe 29/9/2018 na imepanda Ligi Kuu 25/06/2023 miaka mitano ya kupambana kwenye Ligi Daraja la kwanza Championship. Timu hii inaendeshwa kwa ushirikiano wa pande mbili kati ya Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) na Halmashauri ya Manispaa ya Kigoma Ujiji kwa niaba ya Wananchi wa Kigoma. Muelewe hapa maana wengi wanasema ni timu ya Jeshi asilimia 100% Nembo ya timu ni Sokwe Dume, Shujaa wa Hifadhi za Gombe na Mahale zilizopo mkoani Kigoma. Rangi ya kwanza ya jezi ya timu (first kit) ni hiyo hapo chini na kwenye nembo ya timu ni rangi za tunda la michikichi (mawese ). Hii kama njano ni mawese yaliyoganda na huo wekundu ni mawese ya moto. Ukishika tunda la Mse juu utaona wekundu na ukikata katikati utaona njano. Nyeupe ni ‘nazi’ ya Mse hizi ni alama za utajiri wa Kigoma Jezi nyingine ni blue inayowakilisha Ziwa Tanganyika na Jezi nyingine ni Nyeupe

Beno Ngassa mdogo wa Mrisho Ngassa anayekipiga Tanzania Prisons

Miongoni mwa viungo wa pembeni wanaofanya vizuri ni Benodict Khalfan Ngassa ambaye amekuwa akifanya vizuri. Ngassa ambaye ni mtoto wa mchezaji wa zamani wa Pamba Jiji na Simba SC, Khalfan Ngassa, pia ni mdogo wa kiungo mshambuliaji wa zamani wa Yanga, Simba na Azam, Mrisho Ngassa anatajwa ni mmoja kati ya wachezaji wanaotazamiwa kufanya makubwa siku za usoni. Mambo Uwanjani Blog itawaletea Makala maalum ya kiungo huyo hatari ambaye ndoto zake ni kufuata nyayo za kaka yake Mrisho Ngassa. Beno Ngassa