Ruka hadi kwenye maudhui makuu

Tenga: Wachezaji lazima wapimwe


Leodegar Tenga imesema kuna kanuni inayozitaka klabu za Ligi Kuu kuwapima afya wachezaji inaowasajili na kwamba, kinyume na hatua ni kosa.


Klabu za Ligi Kuu Bara zimeendelea kufanya usajili wa wachezaji bila kuwapima afya kama taratibu zinavyotaka, na kwa hali hiyo Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), limesema litaliangalia suala hilo kwa uzito mkubwa.
Kanuni za usajili kama zilivyoainishwa na TFF, inazitaka klabu kuhakikisha zinawapima afya wachezaji wapya wanaowasajili kabla ya kuanza kucheza, jambo ambalo ni kinyume na timu nyingi. Rais wa TFF, Leodegar Tenga alisema jana kuanzia mwaka ujao, hakuna klabu itakayoruhusiwa kusajili wachezaji wapya bila kwanza kuwapima afya na hiyo ni kwa mujibu wa kanuni.
Tenga alisema kanuni ziko wazi kwamba, mchezaji ni lazima apimwe afya kabla ya kusajiliwa, na hii iko kila sehemu mchezo wa soka unakochezwa kwa kiwango cha juu.
“Kuanzia mwaka ujao, TFF haitapokea mikataba ya usajili wa wachezaji  ambayo haitaambatana na taarifa za afya ya mchezaji baada ya kupimwa na klabu anayokwenda kujiunga.
“Kupima afya ya mchezaji kabla ya kumsainisha mkataba ni suala la kikanuni, siyo suala la hiyari na TFF kwa upande wake itahakikisha zoezi hilo linafanyika,” alisema Tenga.
“Kuna mambo mengi yanafanyika kiholela, TFF imejitahidi kwa uwezo wake kuyashughulikia kama msimamizi wa soka,” alisema. Aliongeza: “Tumeanza kutekeleza kwa vitendo kanuni moja baada ya  nyingine na ndiyo maana msimu uliopita tulizibana klabu kuhusu timu B kucheza ligi na hilo lilifanyika.
“Tunafahamu kuna ugumu, hayawezi kutekelezeka yote kwa mara moja lakini tunamaliza moja na kuchukua lingine hadi mpaka tutakapoona klabu  zinaendeshwa kisasa.”
Akizungumzia suala hilo, Meneja Wa Azam FC, Patrick Kahemele alisema  kwa utaratibu wa klabu yao ni lazima wachezaji wa wageni wapimwe afya  zao kabla ya kusajiliwa ndani ya timu.
“Hatujawahi kusajili mchezaji bila kumpima afya, labda awe mchezaji wa  ndani ya timu kwa maana ya kumpandisha daraja kwa sababu wao tayari  wanakuwa wamepimwa,” alisema Kahemele.

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

FIFA yatoa orodha ya vilabu bora duniani, Simba na Yanga zachuana vikali

SHIRIKISHO la Soka Afrika (CAF) limetoa orodha ya viwango vya ubora wa klabu barani, Simba ikiendelea kuwa juu ya klabu nyingine za Tanzania, nafasi ya tano. Orodha hiyo imetoka leo kuelekea droo ya hatua za awali za michuano ya klabu Afrika ambayo kwa mara ya kwanza kihistoria itafanyika nchini katika studio za Azam Tv, Tabata Jijini Dar es Salaam. Yanga ambayo kama Simba itashiriki Ligi ya Mabingwa — yenyewe inashika nafasi ya 12, wakati timu nyingine katika orodha hiyo ni Namungo FC wanaoshika nafasi ya mwisho, ya 75 kwa pamoja na Salitas FC ya Burkina Faso, Ahli Benghazi ya Libya na NAPSA Stars ya Zambia. Kwa msimu ujao mbali na Simba na Yanga kushiriki Ligi ya Mabingwa, Azam FC na Singida Black Stars zitashiriki michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika.

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

Timu inaitwa Mashujaa Lake Tanganyika FC ( Mashujaa FC ) ilianza rasmi kampeni yake ya kupanda Ligi Kuu tarehe 29/9/2018 na imepanda Ligi Kuu 25/06/2023 miaka mitano ya kupambana kwenye Ligi Daraja la kwanza Championship. Timu hii inaendeshwa kwa ushirikiano wa pande mbili kati ya Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) na Halmashauri ya Manispaa ya Kigoma Ujiji kwa niaba ya Wananchi wa Kigoma. Muelewe hapa maana wengi wanasema ni timu ya Jeshi asilimia 100% Nembo ya timu ni Sokwe Dume, Shujaa wa Hifadhi za Gombe na Mahale zilizopo mkoani Kigoma. Rangi ya kwanza ya jezi ya timu (first kit) ni hiyo hapo chini na kwenye nembo ya timu ni rangi za tunda la michikichi (mawese ). Hii kama njano ni mawese yaliyoganda na huo wekundu ni mawese ya moto. Ukishika tunda la Mse juu utaona wekundu na ukikata katikati utaona njano. Nyeupe ni ‘nazi’ ya Mse hizi ni alama za utajiri wa Kigoma Jezi nyingine ni blue inayowakilisha Ziwa Tanganyika na Jezi nyingine ni Nyeupe

Beno Ngassa mdogo wa Mrisho Ngassa anayekipiga Tanzania Prisons

Miongoni mwa viungo wa pembeni wanaofanya vizuri ni Benodict Khalfan Ngassa ambaye amekuwa akifanya vizuri. Ngassa ambaye ni mtoto wa mchezaji wa zamani wa Pamba Jiji na Simba SC, Khalfan Ngassa, pia ni mdogo wa kiungo mshambuliaji wa zamani wa Yanga, Simba na Azam, Mrisho Ngassa anatajwa ni mmoja kati ya wachezaji wanaotazamiwa kufanya makubwa siku za usoni. Mambo Uwanjani Blog itawaletea Makala maalum ya kiungo huyo hatari ambaye ndoto zake ni kufuata nyayo za kaka yake Mrisho Ngassa. Beno Ngassa