Ruka hadi kwenye maudhui makuu

Nyota ya Kaseja yazidi kung'ara, Kibaden akanusha kumtimua

Kocha wa Simba, Abdallah Kibaden 'King'
Kocha wa Simba, Abdallah Kibaden 'King', ameibuka na kukanusha vikali uvumi kwamba ni yeye ndiye aliyemtimua kipa chaguo la kwanza wa timu hiyo na Taifa Stars, Juma Kaseja baada ya kumtema katika orodha ya nyota wanaotarajia kuwamo katika kikosi chake cha msimu ujao wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara.
Badala yake, Kibaden ambaye pia ni mchezaji nyota wa zamani wa 'Wekundu wa Msimbazi' aliyewahi pia kuandika rekodi kwa kuifikisha fainali ya Kombe la Shirikisho wakati akiifundisha mwaka 1993, amefichua kuwa Kaseja hakuwamo katika orodha ya wachezaji aliokabidhiwa na uongozi wa klabu yake hiyo.

Akizungumza  jana, Kibadeni, alisema wakati akikabidhiwa majina ya wachezaji wa timu hiyo ili aanze  kuwanoa, jina la Kaseja halikuwamo na hivyo yeye hawezi kulirejesha kwa maamuzi yake binafsi.
"Sijamkata mimi, ila jina lake sikupewa. Hicho ndicho ninacheweza kukieleza... mambo mengine ni ya ndani ya klabu," alisema Kibaden, mshambuliaji nyota wa zamani wa timu hiyo aliyerejea kuwafundisha baada ya kuihama klabu aliyoiongoza msimu uliopita ya Kagera Sugar.
Alisema kwa sasa tayari ameshapata wachezaji 25 atakaokuwa nao katika msimu ujao wa ligi, huku akiwataja nyota wa kigeni kuwa ni wawili na wote wanatokea Uganda.
"Kikosi changu hakitazidi nyota 25, na wageni hadi leo (jana) ni kipa Abel Dhaira na beki Senkoomi (Samuel), mipango mingine ya ndani ni ya kiufundi. Mazoezi tunayoendelea nayo ni ya kawaida na wengi waliokuja kujaribiwa hawajanishawishi kuwachukua," aliongeza Kibaden.
Akizungumza na mtandao huu jana  Kaseja ambaye aliwahi kusema kitambo kuwa hahofii kutemwa Simba, alisema kuwa hivi sasa anachofanya ni kuendelea kujiweka 'fiti' ili atumikie vizuri taifa kwa sababu yeye na wenzake wa kikosi cha timu ya taifa (Taifa Stars) wana kazi kubwa ya kuhakikisha kuwa wanashinda katika mechi ijayo dhidi ya Uganda na kujiweka katika mazingira mazuri ya kufuzu kwa fainali zijazo za kombe la mataifa ya Afrika kwa wachezaji wa ligi za ndani (CHAN).
"Jamani kuhusiana na Simba siwezi kusema lolote kwa sasa... ila maisha ni popote," alisema nahodha huyo wa Taifa Stars ambaye wiki iliyopita Mambo Uwanjani ilimshuhudia akiwa katika mazoezi ya timu ya vijana ya Simba B, akishauriana na kocha msaidizi wa timu hiyo, Amri Said.
Mwenyekiti wa Simba, Ismail Aden Rage hakutaka kueleza wazi suala la Kaseja na badala yake akasema kuwa hivi sasa, suala la nani asajiliwe na nani aachwe liko katika mamlaka ya kamati yao ya ufundi inayoshirikiana na benchi lao la ufundi.
Rage alisema vigezo vya kusajili mchezaji ni muhimu zaidi kutekelezwa na makocha na kisha kamati ya utendaji itakuwa ya  mwisho kwa lengo la kutoa baraka.

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

FIFA yatoa orodha ya vilabu bora duniani, Simba na Yanga zachuana vikali

SHIRIKISHO la Soka Afrika (CAF) limetoa orodha ya viwango vya ubora wa klabu barani, Simba ikiendelea kuwa juu ya klabu nyingine za Tanzania, nafasi ya tano. Orodha hiyo imetoka leo kuelekea droo ya hatua za awali za michuano ya klabu Afrika ambayo kwa mara ya kwanza kihistoria itafanyika nchini katika studio za Azam Tv, Tabata Jijini Dar es Salaam. Yanga ambayo kama Simba itashiriki Ligi ya Mabingwa — yenyewe inashika nafasi ya 12, wakati timu nyingine katika orodha hiyo ni Namungo FC wanaoshika nafasi ya mwisho, ya 75 kwa pamoja na Salitas FC ya Burkina Faso, Ahli Benghazi ya Libya na NAPSA Stars ya Zambia. Kwa msimu ujao mbali na Simba na Yanga kushiriki Ligi ya Mabingwa, Azam FC na Singida Black Stars zitashiriki michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika.

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

Timu inaitwa Mashujaa Lake Tanganyika FC ( Mashujaa FC ) ilianza rasmi kampeni yake ya kupanda Ligi Kuu tarehe 29/9/2018 na imepanda Ligi Kuu 25/06/2023 miaka mitano ya kupambana kwenye Ligi Daraja la kwanza Championship. Timu hii inaendeshwa kwa ushirikiano wa pande mbili kati ya Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) na Halmashauri ya Manispaa ya Kigoma Ujiji kwa niaba ya Wananchi wa Kigoma. Muelewe hapa maana wengi wanasema ni timu ya Jeshi asilimia 100% Nembo ya timu ni Sokwe Dume, Shujaa wa Hifadhi za Gombe na Mahale zilizopo mkoani Kigoma. Rangi ya kwanza ya jezi ya timu (first kit) ni hiyo hapo chini na kwenye nembo ya timu ni rangi za tunda la michikichi (mawese ). Hii kama njano ni mawese yaliyoganda na huo wekundu ni mawese ya moto. Ukishika tunda la Mse juu utaona wekundu na ukikata katikati utaona njano. Nyeupe ni ‘nazi’ ya Mse hizi ni alama za utajiri wa Kigoma Jezi nyingine ni blue inayowakilisha Ziwa Tanganyika na Jezi nyingine ni Nyeupe

Beno Ngassa mdogo wa Mrisho Ngassa anayekipiga Tanzania Prisons

Miongoni mwa viungo wa pembeni wanaofanya vizuri ni Benodict Khalfan Ngassa ambaye amekuwa akifanya vizuri. Ngassa ambaye ni mtoto wa mchezaji wa zamani wa Pamba Jiji na Simba SC, Khalfan Ngassa, pia ni mdogo wa kiungo mshambuliaji wa zamani wa Yanga, Simba na Azam, Mrisho Ngassa anatajwa ni mmoja kati ya wachezaji wanaotazamiwa kufanya makubwa siku za usoni. Mambo Uwanjani Blog itawaletea Makala maalum ya kiungo huyo hatari ambaye ndoto zake ni kufuata nyayo za kaka yake Mrisho Ngassa. Beno Ngassa