Ruka hadi kwenye maudhui makuu

Ligi Kuu Bara kuanza Agosti 24

Mwenyekiti wa Kamati ya Ligi, Wallace Karia
 
Msimu mpya wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara 2013/2014 utaanza Agosti 24 mwaka huu ambapo timu zote 14 zitashuka dimbani kwenye viwanja tofauti kusaka pointi tatu muhimu, imefahamika.

Akizungumza jana, Mwenyekiti wa Kamati ya Ligi, Wallace Karia, alisema kuwa tarehe hiyo imeshapitishwa katika kalenda ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) na tayari pia mechi za ligi hiyo zimeshapangwa lakini hazijathibitishwa na kamati yake kama taratibu zinavyoeleza.

Karia alisema kuwa tayari 'wataalamu' ambao huhusika na zoezi la kupanga ratiba za mechi wameshakamilisha zoezi hilo lakini kamati yake ndiyo inasubiriwa kupanga siku ya kukutana ili kuithibitisha.

"Ligi itaanza tarehe 24 Agosti ila nani ataanza na nani ndiyo bado hatujapitisha, tukishakutana na kupitia hilo kwa kuzingatia mazingira yetu ya timu kusafiri ndiyo itatolewa hadharani. Tutakuwa makini sana kwa sababu hatutaki makelele yaliyojitokeza mwaka jana na miaka ya nyuma yaendelee," alisema Karia ambaye ameshasema kuwa atawania cheo cha Makamu wa Rais katika uchaguzi ujao wa shirikisho hilo utakaofanyika Septemba.

Hata hivyo, Karia alisema kuwa suala la wadhamini wa ligi hiyo bado halijakamilika lakini kubwa wanachotaka ni kuona ni klabu zinafaidika na udhamini utakaopatikana.

Alisema kuwa kamati yake inatarajia kukutana Julai 3 asubuhi ili kupitia taarifa za msimu uliopita na kupata washindi wa tuzo mbalimbali na jioni yake washindi hao watatangazwa na kutunukiwa.

"Tumepanga tukutane siku hiyo hiyo ya tuzo ili habari zisivuje, kwa sababu kila mtu na kifua chake cha kuweka mambo…  hadi sasa ni bingwa, mshindi wa pili na wa tatu ndiyo wanajulikana. Lakini kocha bora na tuzo nyingine tutajua siku hiyo baada ya kuangalia na kuthibitisha rekodi tulizonazo," aliongeza Karia.

Kabla ya kuanza kwa ligi hiyo, bingwa mtetezi Yanga na mshindi wa pili, Azam watakutana katika mechi ya kuwania Ngao ya Jamii kama kanuni za ligi zinavyosema.

Timu 14 za msimu ujao wa ligi ni pamoja na Yanga, Azam, Simba, Kagera Sugar, Mtibwa Sugar, Coastal Union, JKT Oljoro, JKT Ruvu, Ruvu Shooting, Mgambo Shooting, Prisons na zilizopanda daraja ambazo ni Mbeya City, Ashanti na Rhino Rangers ya Tabora.

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

FIFA yatoa orodha ya vilabu bora duniani, Simba na Yanga zachuana vikali

SHIRIKISHO la Soka Afrika (CAF) limetoa orodha ya viwango vya ubora wa klabu barani, Simba ikiendelea kuwa juu ya klabu nyingine za Tanzania, nafasi ya tano. Orodha hiyo imetoka leo kuelekea droo ya hatua za awali za michuano ya klabu Afrika ambayo kwa mara ya kwanza kihistoria itafanyika nchini katika studio za Azam Tv, Tabata Jijini Dar es Salaam. Yanga ambayo kama Simba itashiriki Ligi ya Mabingwa — yenyewe inashika nafasi ya 12, wakati timu nyingine katika orodha hiyo ni Namungo FC wanaoshika nafasi ya mwisho, ya 75 kwa pamoja na Salitas FC ya Burkina Faso, Ahli Benghazi ya Libya na NAPSA Stars ya Zambia. Kwa msimu ujao mbali na Simba na Yanga kushiriki Ligi ya Mabingwa, Azam FC na Singida Black Stars zitashiriki michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika.

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

Timu inaitwa Mashujaa Lake Tanganyika FC ( Mashujaa FC ) ilianza rasmi kampeni yake ya kupanda Ligi Kuu tarehe 29/9/2018 na imepanda Ligi Kuu 25/06/2023 miaka mitano ya kupambana kwenye Ligi Daraja la kwanza Championship. Timu hii inaendeshwa kwa ushirikiano wa pande mbili kati ya Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) na Halmashauri ya Manispaa ya Kigoma Ujiji kwa niaba ya Wananchi wa Kigoma. Muelewe hapa maana wengi wanasema ni timu ya Jeshi asilimia 100% Nembo ya timu ni Sokwe Dume, Shujaa wa Hifadhi za Gombe na Mahale zilizopo mkoani Kigoma. Rangi ya kwanza ya jezi ya timu (first kit) ni hiyo hapo chini na kwenye nembo ya timu ni rangi za tunda la michikichi (mawese ). Hii kama njano ni mawese yaliyoganda na huo wekundu ni mawese ya moto. Ukishika tunda la Mse juu utaona wekundu na ukikata katikati utaona njano. Nyeupe ni ‘nazi’ ya Mse hizi ni alama za utajiri wa Kigoma Jezi nyingine ni blue inayowakilisha Ziwa Tanganyika na Jezi nyingine ni Nyeupe

Beno Ngassa mdogo wa Mrisho Ngassa anayekipiga Tanzania Prisons

Miongoni mwa viungo wa pembeni wanaofanya vizuri ni Benodict Khalfan Ngassa ambaye amekuwa akifanya vizuri. Ngassa ambaye ni mtoto wa mchezaji wa zamani wa Pamba Jiji na Simba SC, Khalfan Ngassa, pia ni mdogo wa kiungo mshambuliaji wa zamani wa Yanga, Simba na Azam, Mrisho Ngassa anatajwa ni mmoja kati ya wachezaji wanaotazamiwa kufanya makubwa siku za usoni. Mambo Uwanjani Blog itawaletea Makala maalum ya kiungo huyo hatari ambaye ndoto zake ni kufuata nyayo za kaka yake Mrisho Ngassa. Beno Ngassa