KONE KUTUA WIGAN, ADAI ANATAKA KWENDA KWA MARTINEZ

Get me to Goodison: Arouna Kone wants to rejoin former manager Roberto Martinez at EvertonMSHAMBULIAJI Arouna Kone anayetaka kuondoka amewaambia Wigan anataka kusaini Everton akiondoka Uwanja wa DW.
Timu zote, Norwich na Swansea ziko tayari kulipa Pauni Milioni 6 kuununua Mkataba wa mchezaji huyo.
Lakini nyota huyo wa Ivory Coast anataka kuungana na kocha wake wa zamani, Roberto Martinez, ambaye amehamia Goodison Park mwezi uliopita.
Alikuwa Martinez aliyemvuta Kone, mwenye umri wa miaka 29, England miezi 12 iliyopita kwa Pauni Milioni 3.5 kutoka Levante.
Na mshambuliaji huyo anaamini Mspanyola huyo anaweza kumfanya aendelee kuwa bora katika Ligi Kuu ya England.

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

FIFA yatoa orodha ya vilabu bora duniani, Simba na Yanga zachuana vikali

Beno Ngassa mdogo wa Mrisho Ngassa anayekipiga Tanzania Prisons

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI