Urusi yaikabidhi Syria 'zana za kivita'

Urusi yaikabidhi Syria 'zana za kivita'


Makombora

Syria imepokea ngao za kwanza kutoka kwa Urusi, za kuikinga nchi hiyo dhidi ya mashambulizi ya makombora ya angani. Hii ni kwa mujibu wa rais wa nchi hiyo, Bashar al-Assad.

Urusi imeahidi kuendelea na mpango wake wa kuhami Syria, mara tu baada ya uamuzi wa muungano wa Ulaya wa kuondolea nchi hiyo vikwazo vya silaha.
Bwana Assad pia anaripotiwa kuambia televisheini yenye uhusiano na kundi la Hezbollah, kuwa sasa kumekucha kwani vita ndio vinaanza kushika kasi.
Awali, kiongozi mmoja wa waasi aliambia BBC kuwa Hezbollah imekuwa ikishambalia Syria.
Generali Selim Idriss, kwenye mahojiano na BBC alisema kuwa zaidi ya wapiganaji 7,000 wa kishia kutoka Lebanon, wanashiriki vita dhidi ya utawala wa Syria mjini Qusair, mji ambao unadhibitiwa na waasi.
Mfumo wa S-300 ni wa hali ya juu ambao unaweza kukinga makombora ya angani na ya sakafuni.
Hatua ya Urusi kuikaibidhi Syria zana kama hizo, inazua wasiwasi zaidi hasa baada ya Syria kusema kuwa itajibu mashambulizi yoyote kutoka kwa Israel, msimamo ambao pia umechukuliwa na Urusi.
Wadadisi wanasema kuwa huenda pande zinaojihusisha na mzozo wa Syria zikaanza kutumia makombora kwenye vita hivi.
Pia inahofiwa kuwa mashambulizi ya makombora yanaweza kutishia juhudi za kuandaa mkutano wa amani kuhusu Syria mjini Geneva mwezi Juni.
Waziri wa mambo ya nje wa Syria amesema kuwa majeshi ya nchi hiyo sasa yamerejea katika hali nzuri ya kupambana na waasi.

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

STAA WETU: JEREMIA JUMA MTOTO WA JUMA MGUNDA ALIYEIKACHA SIMBA NA KUENDELEA NA UASKARI

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA