NEYMAR AMWAGA 'MACHOZI DEBE' AKIICHEZEA MECHI YA MWISHO SANTOS


MSHAMBULIAJI Neymar alimwaga machozi usiku wa kuamkia leo, wakati akiichezea klabu yake, Santos mechi ya mwisho kabla ya kuhamia Barcelona.
Nyota huyo wa Brazil atakayejiunga na vigogo hao wa Catalan kwa mkataba wa miaka mitano msimu ujao aliiaga  klabu yake iliyomlea kisoka kwa sare ya 0-0 na Flamengo.
Katika taarifa yake aliyotoa jana kwenye Instagram, alifafanua ni kiasi gani hatawasahu mashabiki wa Santos ambayo iko moyoni mwake. 
Saying goodbye: Neymar was visibly upset before his final outing for Santos
Kwaheri: Neymar alikuwa mpweke kabla ya kuichezea Santos mechi ya mwisho
Saying goodbye: Neymar was visibly upset before his final outing for Santos
Saying goodbye: Neymar was visibly upset before his final outing for Santos
VIDEO: Neymar akisalimiana kabla ya mechi
 
Neymar aliandika: "Nataka kuwashukuru mashabiki wa Santos kwa miaka tisa mizuri. Hisia zangu kwa klabu na mashabiki hazitabadilika!
"Ni klabu kama Santos FC pekee inaweza kunipa kila kitu nilichojifunza ndani na nje ya Uwanja. Nawashukuru mashabiki baab kubwa, ambao wamenisapoti hata katika wakati mgumu.
"Mataji, mabao, chenga, ushangiliaji na nyimbo mashabiki walizotunga kwa ajili yangu vitadumu daima moyoni mwangu...'
Neymar's message

WASIFU WA NEYMAR

Neymar
1992: Februari 5 - Alizaliwa mjini Mogi das Cruzes, Brazil.
2003: Alijiunga na akademi ya Santos.
2006: Alikwenda Hispania kufanya majaribio Real Madrid, lakini akaamua kubaki Santos.
2009: Machi - Aliichezea mechi ya kwanza Santos akiwa na umri wa miaka 17 kabla ya kuifungia bao lake la kwanza timu ya wakubwa wiki moja baadaye.
2010: Aprili 15 - Alifunga mabao matano Santos ikiifunga Guarani 8-1.
Mei - Aliteuliwa Mchezaji Bora wa Campeonato Paulista huku Santos ikishinda taji.
Julai - Mkurugenzi wa Soka wa Santos, Pedro Luiz Nunes alisema klabu ilikataa ofa ya Pauni Milioni 12 kutoka West Ham. Neymar pia alikanusha amekubali kujiunga na Chelsea.
Agosti 10 - Alifunga bao akiichezea Brazil kwa mara ya kwanza ikiibuka na ushindi wa 2-0 katika mchezo wa kirafiki dhidi ya Marekani.
Desemba 30 - Alikuwa wa tatu katika kura za uteuzi wa Mwanasoka Bora wa Mwaka Amerika Kusini, baada ya kufunga mabao 42 katika mechi 60.
2011: Juni - Alifunga wakati Santos ikitwaa taji la Copa Libertadores kwa mara ya kwanza tangu mwaka 1963 - wakati Pele bado anaichezea klabu hiyo.
Novemba - Alisaini mkataba mpya na Santos kuendelea kuichezea hadi baada ya Kombe la Dunia 2014 Brazil.
Desemba - Aliteuliwa kuwania tuzo ya Mwanasoka Bora wa Dunia wa FIFA na akashinda tuzo ya Puskas kutokana na bao lake dhidi ya Flamengo.
Alishinda Medali ya Shaba katika Klabu Bingwa ya Dunia, Santos ikifungwa na Barcelona 4-0 katika Fainali.
Desemba 30 - Alishinda tuzo ya Mwanasoka Bora wa Mwaka Amerika Kusini.
2012: Februari 5 - Alifunga bao lake la 100 katika timu ya wakubwa, akisherehekea kutimiza miaka 20 ya kuzaliwa katika mechi dhidi ya Palmeiras.
Mei - Alifunga mabao mawili kwa miguu yote kwenye Fainali ya Campeonato dhidi ya Guarani, Santos ikishinda 7-2 jumla.
Juni- Aliibuka mfungaji bora wa Copa Libertadores, lakini Santos ilifungwa katika Nusu Fainali na Corinthians.
Desemba - Alishinda tuzo ya Mwanasoka Bora wa Mwaka wa Amerika Kusini kwa mara ya pili, wakati pia alishinda Kiatu cha Dhahabu kama mchezaji bora katika michuano ya ubingwa wa Brazil. Alikanusha kuwa na mpango na Barcelona.
2013: Machi 18 - Alisema kucheza Ulaya ni ndoto yake.
Aprili 25 - Baba yake na wakala wake, Neymar da Silva Sr, alisema Neymar ataondoka Santos kabla ya Kombe la Dunia mwakani, 2014.
Mei 25 - Santos ilitangaza kukubali ofa mbili kwa ajili ya mshambuliaji huyo, moja ya Real Madrid na nyingine Barcelona.
Mei 26 - Neymar na Barcelona wanathibitisha amechagua kujiunga na mabingwa hao wa Hispania.

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA

STAA WETU: JEREMIA JUMA MTOTO WA JUMA MGUNDA ALIYEIKACHA SIMBA NA KUENDELEA NA UASKARI